AKAMATWA KWA MAUAJI YA MZAZI MWENZAKE!

 AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWENZA WAKE.

Na. Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Arusha.



Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia ,John Maganga (26) mlinzi, mkazi wa Makumira wilaya ya Arumeru kwa tuhuma za mauaji ya Safina Emanuel (19) mama lishe na mkazi wa Magadirisho wilayani humo.


Akitoa taarifa hiyo Disemba 21, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo  amesema mwili wa marehemu ulipatikana maeneo ya Makumira kando ya barabara ya Moshi- Arusha.


Kamanda Masejo ameendelea kufafanua kuwa mara baada ya kuupata mwili huo walianza upelelezi na kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye ni mzazi mwenza wa marehemu na kukiri kuhusika katika tukio hilo Disemba 19, 2024, pia kueleza namna ambavyo aliuficha mwili huo.


Aidha amesema kuwa wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo na pindi utakapokamilika taratibu nyingine za kisheria zitafuata.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema litaendelea kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria kwa watu wote watakaojihusisha na vitendo vya uhalifu. Pia limewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu.

Post a Comment

0 Comments