Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WAZIRI wa Maliasili na Utali, Balozi Dk Pindi Chana ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma na Misitu (TFS) kuhakikisha idara hiyo inajikita katika kukusanya mapato kupitia mifumo ya kisasa yaTehama ili idara hiyo iongeze mapato ya serikali.
Waziri Chana ametoa agizo leo Novemba 5,2024 wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa Makamanda wa TFS jijini Arusha.Ambapo pamoja na mambo mengine ameikumbusha TFS wajibu wao wa kulinda misitu hapa nchini.
Alisema pamoja na kuvuka malengo waliojiwekea na kukusanya mapato ya Sh bilioni 166 sawa na asilimia 103, kama wangekuwa wanatumia mfumo wa Tehama malengo hayo yangekuwa makubwa zaidi kuliko ilivyo sasa.
Pamoja na kuipongeza TFS kwa kuvuka malengo ya makusanyo ila alisisitiza taasisi hiyo kukusanya mapato kwa mfumo wa Tehama kwani idara nyingi za serikali zimejikita katika mfumo huo ikiw ani pmaoja na kuunganisha migumo yoa iweze kuonana na taasisi zingine za serikali.
Waziri Chana alisema hadi Juni mwaka huu, TFS ilikusanya zaidi ya Sh bilioni 166 na kuvuka malengo yaliyokusudiwa.
“Hivyo pongezi za dhati kwa menejimenti chini ya Kamishina Silayo na bodi lakini jitihada zaidi zinahitajika"
Alisema sifa kuu ya askari kwanza ni kuwa mzalendo, muadilifu na muaminifu hivyo makamanda wa TFS wanapaswa kwenda sambamba na misingi hiyo ili kulinda misingi ya kazi katika uendeshaji kazi za kila siku ili serikali iendelee kuwaamini.
Alisema TFS inapaswa kufanya kazi kisasa ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kununuwa vitendea kazi vya kisasa ikiwa ni pamoja na magari ya kisasa, ndege na helkopta vyote vinahitajika katika utendaji kazi wa ulinzi wa misitu.
Waziri huyo aliitaka menejimenti na Bodi ya TFS kuhakikisha wanatatua changamoto za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kupigania maslahi yao na kupandishwa madaraja wanayostahili.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TFS, Brigedia Jeneral Mbaraka Naziad Mkeremy alisema kuwa TFS imejipanga kuhakikisha malengo ya makusanyo ya kila mwaka yanafikiwa na kuzidi ili taasisi hiyo iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi na kuhakikisha taasisi hiyo inatatua changamoto za jamii.
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi, Mhandisi Enock Nyanda ambaye ni mjumbe wa Bodi ya TFS na kusisitiza kuwa Bodi hiyo itashirikiana na menejimenti katika kuhakikisha inajali maslahi ya wafanyakazi wafanyakazi na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mwenyekiti wa Bodi alisema kuwa TFS imekuwa ikishirikiana na jamii katika kutatua changamoto lengo ni kutaka jamii kuishi kwa kufata kanuni na sheria za misitu na nyuki.
Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo alisema lengo la kikao hicho ni kujengeana uwezo wa utendaji kazi, kubadilisha uzoefu, kujadiliana na kushauriana kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za utendaji kazi ili kuimarisha mifumo ya utendaji kazi.
Alifafanua kuwa pamoja na mambo mengine kikao hicho kitatoa mada kuhusu Intelijensia ya mawazo, fikra za kimkakati, kujenga uwezo wa kuongoza, usimamizi wa sekta ya misitu , mbinu za uongozi, usimamizi wa sera na sekta ya ufugaji nyuki, changamoto na mwelekeo wake.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Washiriki takribani 240 ikijumuisha Viongozi wa Kanda zote Saba za TFS pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya TFS, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Deusdedit Bwoyo, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Menejimenti ya TFS, Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa Mashamba na Wilaya wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Ends
0 Comments