WANANCHI WATISHIA KULIAMSHA BAADA YA MGOMBA WAO WA CCM KUKATWA JINA ,JINA LA REJESHWA CHAP SASA ATAGOMBEA KWA KISHINDO KUTETEA NAFASI YAKE YA MWENYEKITI WA MTAA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Taharuki ya kuogofya imeibuka kwa wananchi na wafuasi wa ccm katika mtaa wa Olkung'u kata ya Terat jijini Arusha mara baada ya jina la mgombea wa chama hicho,Daud Mollel anayetetea nafasi yake ya Mwenyekiti wa mtaa huo kukatwa na wananchi kutishia kuliamsha kwa maandamano. 

Hata hivyo mgombea huyo akiwa na wafuasi wake waliamua kutinga katika ofisi ya Mtendaji wa kata hiyo kuhoji namna jina lake lilivyoyeyuka ndipo walipoelezwa  kwamba jina lake  lilikosewa katika hatua za uchapaji ila litafanyiwa marekebisho na kurejeshwa kama   mgombea.


Akiongea na vyombo vya habari katibu wa ccm wa kata hiyo ya Terat,Bartazal Milinga alisema wakati wanahakiki majina ya wagombea walibaini kwamba jina la mgombea wao katika mtaa wa Olkung'u Daud Mollel halipo ndipo wananchi walipozua taharuki na kujipanga kuandamana.

Milinga alisema waliamua kufuatilia ofisi ya mtendaji kata kuhoji kilichotokea kati ya mitaa nane ya kata hiyo jina la mgombea wa mtaa mmoja wa Olkung'u halikurudi na kubaini kwamba majina yake yalitofautiana na majina aliyojaza kwenye fomu ya chama na yaliyopo kwenye fomu ya kugombea.

Alisema suala hilo linashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria ili aweze kugombea nafasi hiyo kwa sababu chama kinaimani haye na wananchi  wanamhitaji .


Akiongelea taharuki hiyo mgombea ,Daud Mollel alisema amefarijika kuona jina lake linarejeshwa na atashiriki kama mgombea wa nafasi hiyo na kuwasihi wafuasi wake watulie kwa kuwa suala hilo linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Alisema jina lake lilikosewa katika uchapaji ndio maana walishindwa kuelewa jina halisi la mgombea ni lipi ila kwa sasa anajisikia amani baada ya kuhakikishiwa kuwa jina lake litarekebishwa na atashiriki kutetea nafasi yake ya Mwenyekiti wa mtaa wa olkung'u.

Ends...


Post a Comment

0 Comments