WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAJADILI MAMBO MAZITO ARUSHA ,RAIS SAMIA AKOMALIA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

WAKUU wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)  wamekutana jijini Arusha kujadiliana masuala mbalimbali muhimu ikiwemo kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi, uzalishaji wa bidhaa na masoko ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi wanachama na masuala ya ulinzi na usalama. 

Viongozi hao walikutana pia katika maadhimisho ya miaka 25 ya EAC ambayo ilianishwa mwaka 1999. Kabla ya kuanzishwa, jumuiya hiyo ilikuwapo kuanzia mwaka 1967 kabla ya kuvunjika mwaka 1977.



Rais Samia Hassan Suluhu alizitaka nchi za EAC kuunga mkono jitihada za matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuwezesha wanawake kutopata madhara kiafya sambamba na vijana kupata ajira hususan wa vijijini kwa kupata umeme wa uhakika.  



Pia alisema mabadiliko ya tabianchi yana athari kubwa katika nchi, hivyo Tanzania imejipanga kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanakuwa kwa kasi katika  maeneo ya vijijini na mijini.  


Alisema Tanzania  inajitahidi kupambania matumizi ya nishati safi ya kupikia na inahitaji zaidi ya dola milioni  19 katika kipindi cha miaka mitano kwa ajili ya kurekebisha masuala la mazingira, hivyo  kila wilaya nchini Tanzania iendelee kupanda miti ingawa kasi yake ni ndogo. 







"Tanzania imejipanga kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia yanakua ikiwamo kupunguza wimbi la vijana kukimbia mjini kwani hivi sasa wanapata ajira huko vijijini na kinamama kutumia nishati ya umeme." 


Alisema wanawake wanapata matatizo mbalimbali kutokana na matumizi ya kuni hivyo lazima kuhakikisha wanawake wanaondoka na matumizi ya nishati hiyo nawaomba wakuu wa nchi waniunge mkono kuhakikikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.


 Tanzania, alisema  imekuja na sera ya upandaji  miti kila mwaka kwa kila wilaya lakini bado kasi haijakuwa nzuri.









                               





Katika mapambano ya nishati chafu Tanzania inapambana si kuhakikisha inasambaza umeme vijijini ili kuwezesha wanawake kupikia, ikiwamo vijana kujiajiri ikiwamo kusambaza umeme wa gesi, kwani nusu ya umeme wa Tanzania unatokana na maji ikiwamo mabwawa ya maji.  



Alisema katika suala la mabadiliko ya tabianchi, lazima kila nchi ya EAC kukubaliana kwa pamoja ili kuunganisha nguvu na kusisitiza nchi hizo  kushirikiana na sekta binafsi ili kuwezesha matumizi ya nishati hivyo yanakuwa kwa kasi.



 Alisema ukosefu wa ajira na nyenzo za vijana kujipatia ajira hivyo Tanzania imekuja na mpango wa BBT kwa kuhakikikisha vijana wanajiajiri katika kilimo na mipango mingine ya kisera ikiwamo kilimo, mifugo na misitu hivyo Tanzania imetengeneza uwanda mpana kwa vijana ili wajue kilimo ni ajira.  


Alisema tatizo kubwa la vijana ni  kupata ardhi, fedha, teknolojia hivyo serikali ya Tanzania imetenga maeneo makubwa mfano Dodoma kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ikiwamo utoaji wa ardhi na hati ikiwamo kujengewa makazi na kuunganishwa katika mnyororo wa soko ikiwamo uunganishaji wa vijana na benki ili kutoa mikopo kwa vijana kwa ajili ya kilimo. 



Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, alisema ni vyema  kuongeza uwezekano wa mazao  ya kilimo, uvuvi, viwanda na mifugo, kufikia masoko mapana kwani sekta hizo ni muhimu kwa uchunguzi lakini pia miradi ya kikanda katika uchukuzi na uunganishaji wa nishati katika kuipatia  Somalia fursa ya kuimarisha miundombinu na  kuunganisha masoko. 


Huku Rais William Ruto wa Kenya alisisitiza umuhimu wa amani na utulivu katika pembe za Afrika ikiwamo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kuisaidia zaidi nchi ya Congo katika masuala ya amani. 


Alisisitiza kipaumbele zaidi katika kuimarisha mikataba ya biashara kwa kuanzisha mikataba mipya inayoimarisha kilimo na miundombinu ikiwamo kusaidia wafanyabiashara wa viwanda vidogo na vya kati na  utoaji mafunzo na rasilimali kwa wawezekaji haswa maeneo ya mipakani. 



Naye Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombaza, alisisitiza kipaumbele zaidi katika kuimarisha mikataba ya biashara ikiwamo ile inayoimarisha kilimo na miundombinu na kusaida wafanyabiashara wa viwanda vidogo na vya kati kwa utoaji mafunzo na rasilimali kwa wawezekaji hasa maeneo ya mipakani.








Post a Comment

0 Comments