VIONGOZI WA DINI ARUSHA,WAPONGEZA TUME YA UCHAGUZI KWA KUANZA MCHAKATO MAPEMA WA UCHAGUZI,WATAKA IPELEKE ELIMU YA KUBIRESHA DAFTARI LA MPIGA KURA VIJIJINI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


VIONGOZI wa dini Mkoani Arusha,wameipongeza Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi nchini (INEC), namna inavyoshirikisha makundi mbalimbali kwa lengo la kuelimisha na kukusanya maoni ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kuiunga mkono tume hiyo kwa kuhamasisha jamii.
 

Msemaji wa Taasisi kongwe ya kiislamu ya Twariqa Qadiriya Razikia Jailania Tanzania,  makao Makuu Arusha,Sheikh Haruna Huseni aliwaomba viongozi wa dini , wanasiasa na viongozi wa mila kuungana kwa pamoja na kuhamasisha jamii kwenda  kuboresha taarifa zao muhimu katika daftari la kudumu la mpiga kura kama takwa la kisheria linavyosema.

Sheikh Haruna aliiomba tume ya uchaguzi kuendelea kutoa elimu hiyo kwa uwazi zaidi hasa katika maeneo mengine hususani yale ya vijijini ambayo yamekuwa hayafikiwi kwa mapana yake.

"Niwaombe wananchi tujitokeze kuweka taarifa zetu sawa  kwa wale waliohamia kutoka eneo moja hadi nyingine na wale watakaotimiza umri wa miaka 18 hao pia ni wadau muhimu sana  katika kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025 Kama kauli mbiu inavyosema, uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mwaka 2024/25 ni kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora"Alisema.

Pia aliomba tume kuwajengea mazingira salama makundi ya walemavu  na wajawazito kuweza  kupata elimu hiyo ambayo ni muhimu sana wakati taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2025.

Naye Mchungaji wa kanisa la Moraviani, Yohane Parkipumi alimshukuru Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kuilinda na kudumisha amani iliyoasisiwa na watangulizi wake.

Mchungaji huyo aliwaomba wachungaji,Masheikh na viongozi wa mila kuendelea kuliombea taifa hasa wakati nchi inaelekea kufanya uchaguzi mwakani.

"Watanzania wote tujitokeze kushiriki kikamilifu kuboresha taarifa zetu kwenye daftari la kudumu la mpiga kura wakati utakapofika"

Naye sheikh Iddy Ngella alipongeza mahusiano mazuri baina ya Taifa la Tanzania na Majirani zake yanayijengwa na wakuu wa hicvi hizo na kutoa rai kwa watanzania hususani wakazi wa Arusha kutumia amani hiyo kukuza uchumi wa taifa letu na kipato cha mtu mmoja mmoja.








Enda..









Post a Comment

0 Comments