VIONGOZI WA DINI ARUSHA WAGEUKIA UTALII WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA ,WATAPANDA MITI 10,000

Na Joseph Ngilisho,ARUSHA 

Kamishna msaidizi wa uhifadhi Kitengo cha Maendeleo na Biashara ,Tanapa,Jully Lyimo kushoto  na msemaji wa Twarika Sheikh Haruna Husein wakizindua jezi ya kuhamasisha utalii 

VIONGOZI wa dini  Mkoa wa Arusha wameanza kampeni ya kuhamasisha utalii na  upandaji wa miti ,na kwa kuanzia  wamepanga kupanda miti 10,000 ikiwa ni mpango wa kuboresha mazingira katika maeneo ya akiba na  mpango huo unapaswa kuigwa na viongozi wote wa dini nchini.

Kamishna msaidizi wa uhifadhi Kitengo cha Maendeleo na Biashara ,Tanapa,Jully Lyimo alibainisha hayo jijini Arusha wakati alipokuwa akiongea na viongozi wa dini katika hafla ya uzinduzi wa Tisheti Mpya iliyoandaliwa na taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika, iliyolenga kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kauli mbiu isemayo 'Viongozi wa dini uhifadhi endelevu'.


Lyimo alisisitiza kuwa viongozi wa dini waendelee kuwamasisha waumini wao kuhusu utalii wa ndani jambo litakalosaidia  kuongeza uelewa kuhusu uhifadhi endelevu.


"Viongozi wa dini mmekuwa mfano wa kuigwa kwa kufuata nyayo za Rais wetu Samia Suluhu Hasan ambaye amekuwa mhifadhi wa kwanza kupitia filamu yake ya The Royal Tour"


Aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuwahamasisha waumini wao ili kuweza kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini.


Alisema Tanapa itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika kukuza sekta ya utalii hapa nchini.


Awali kiongozi wa Twarika Sheikh Haruna Husein ,alisema kuwa wajibu wa viongozi wa dini  ni pamoja na kuelezea umuhimu wa sekta ya utalii katika kukuza uchumi wa Taifa .


Alisema viongozi wa dini wanawajibu wa kumuunga mkono rais Samia ambaye amekuwa rais wa kwanza kuhamasisha utalii kupitia filamu ya Rayol Tour ambayo aliicheza mahususi kutangaza vivutio vyetu hapa nchini.


Naye Mchungaji Zelothe Palangyo alisema viongozi wa dini wameamua kumuunga mkono Rais Samia kupitia utunzaji wa mazingira kwa kuamua kuanzisha kampeni ya upandaji miti.


Viongozi hao wa dini wamempongeza pia raia Samia kwa kampeni ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kuhamaisha matumizi ya nishati ya desi.








Ends..














Post a Comment

0 Comments