Na Joseph Ngilisho ARUSHA
DUKA Maarufu linalojihusisha na uuzaji wa vifaa vya umeme katika jiji la Arusha la UMEME PLUS limezindua kampeni mpya ya msimu wa sikukuu, itakayowanufaisha wateja ikiwa ni pamoja na kupata punguzo kwa asilimia kubwa.
Akiongea na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa UMEME PLUS, Roman Shayo alisema kampeni hiyo itawashirikisha pia watengenezaji wa Maudhi kwenye mitandao ya kijamii.
Alisema kampeni hiyo imelenga kuwatambua na kuwapa hadhi ya RED CARPET wateja wake ili watakapofika katika duka hilo watapita kwenye zuria Jekundu(red-carpet)ikiwa ni hadhi ya juu ya kuthamini mteja kama mfalme .
"Tumeamua katika kipindi cha msimu wa sikukuu tuwatambue na kuwapatia hadhi ya Red-carpet wateja wetu watakuwa wakipita kwenye zuria jekundi kama ambavyo viongozi wa juu wa serikali wanavyoheshimiwa"Alisema Shayo...
Alisema wanatumia fursa hiyo kuwaalika watu wenye ushawishi kushiriki uzoefu wao na bidhaa zao za dukani kwenye mitandao ya kijamii.
"Katika kuelekea msimu wa sikukuu tumejipanga kuanzisha mashindano ya mchezo wa Pool table ili kuibua vipaji vya ndani na nje ya jiji la Arusha katika eneo ambalo UMEMEPLUS itafunga taa za kisasa zenye mvuto ili kuonesha ujuzi na ufundi wa mchezo huo"
Alisema vijana watapata fursa ya kushiriki CHALLENGE ya kuonesha nyumba bora ya kuishi iliyopangiliwa vizuri (YOUTH BADASS GHETTOS) kwa kurekodi video fupi na kuituma mtandaoni na kuwaalika wafuasi wao kwa ku-comment .
"Tunawaalika vijana na watu binafsi wenye nyumba nzuri kushiriki challenge ya kuonesha nyumba zao kwenye mtandao na Mshindi atapata huduma ya kuboreshewa kwa kufungiwa taa nzuri nyumbani kwake "
Mkurugenzi Shayo alisema Kampeni hiyo itawafikia pia viongozi wa dini ,wachungaji na Masheikh kwa kushiriki katika challenge hiyo.
Alisema Duka la UMEME PLUS limejitolea kutoa vifaa vya umeme na suluhu ya taa zenye ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia ubunifu wa kuridhika kwa wateja kupitia teknolojia ya kisasa.
0 Comments