Na Joseph Ngilisho ARUSHA
ZOEZI la upigaji kura linalofanyika leo nchini Tanzania katika uchaguzi wa serikali za mitaa,Wananchi wa Kata ya Ngarenaro wameitika hususani vijana na akina mama kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi kuwachagua viongozi wanaowataka.
Mbali na changamoto kadhaa za baadhi ya wapiga kura kutoona majina yao mwitikio na morari kwa wapiga kura ni mkubwa.
Hata hivyo katika kituo cha Engasengiu kata ya Sinoni, Mmoja ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti Damiano Mollel(CHADEMA)amejikuta akiangua kilio baada ya kukosa jina lake kwenye kituo cha kura.
Kata ya Ungalimited mtaa wa Darajani ,baadhi ya vituo havina mawakala wa vyama vya upinzani, jambo ambalo limelalamikiwa na wagombea.
Katika kata ya Murieth ,mtaa wa NADOKATI Masanduku ya kura yamechelewa kufika hadi majira ya saa 10 asubuhi wananchi walikuwa bado kupiga kura
Ends.
0 Comments