Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Wakazi takribani 40 wa mtaa wa Nadosoito kati, kata ya Muriet jijini Arusha wamehamishia makazi yao katika mahakama jumuishi Mkoani Arusha wakiituhumu mahakama hiyo kutowatendea haki katika maamuzi yake baada ya kuamuru nyumba zao 13 kubomolewa kinyume na utaratibu na wao kukosa mahala pa kuishi .
Akiongea kwa niaba ya wenzake ,Olodi Laizer, alisema "sisi na watoto wetu tumeamua kuja kulala hapa mahakamani baada ya mahakama kuamuru tubomolewe nyumba zetu na sisi kukosa mahala pa kuishi katika kesi ambayo haituhusu "
Alisema kesi hiyo ilikuwa kati ya mlalamikaji, Fanuel Noar na Godfrey ole Martin iliyoanza mwaka 1993.
Alisema julai mwaka huu ,Mahakama ilitoa hukumu na kumpatia ushindi mlalamikaji na baadaye amri ya kulitwaa eneo hilo ilitolewa na nyumba 13 zilivunjwa na wao kama waathirika wa tukio hilo waliamua kuendelea kuishi katika eneo hilo kwa kujisitiri na maturubai baada ya kukosa pa kuishi ila juzi walivamiwa na askari wa kampuni binafsi ya ulinzi na kuwatimua.
"Kesi ilipomalizika upande ulioshinda walikaza hukumu na mahakama ilitoa oda ya utekelezaji ,na katika amri ya utekelezaji walioshinda walipaswa kutekeleza eneo lenye ukubwa wa ekari 15 pekee,lakini dalali wa mahakama alijitwalia eneo zaidi la ekari 49 na kuvunja nyumba 13 zikiwemo za kwetu tusiohusika"
"Niliandika barua ya malalamiko kuiomba mahakama kwenda kujiridhisha na utekelezaji wa oda ya mahakama kwa sababu wali unja eneo lisilohusika na mgogoro huo"
Wananchi hao wakiwa na watoto wadogo na wanafunzi,walidai kwamba waliamua kutinga katika mahakama hiyo baada ya kufukuzwa na kuchomwa moto kwa mahema waliokuwa wamejihifadhi ,na hivyo wanaishinikiza mahakama iwatendee haki kwani hadi sasa tangia wavunjiwe nyumba zao na dalali wa mahakama julai mwaka huu hawana mahala pa kuishi .
Alisema siku hiyo baada ya kufika eneo la mahakama wkaijiandaa kulala,walivamiwa na polisi na kwenda kuwekwa lokapu lakini mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa alifanikisha kuwatoa na kwenda kuwapatia hifadhi ya kulala katika ofisi yake ila asubuhi walirejea katika mahakama hiyo.
"Hadi sasa unapotuona sisi na watoto hatujala chochote na watoto wanalia njaa, hawajaenda shule na hakuna aliyekuja kutusikiliza"
Olodi alimwomba Rais Samia suluhu Hasan kuingilia hati ili haki yetu ipatikane kwani tunaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yetu na tutaendelea kuishi hapa mahakamani hadi hapo tutakapopata msaada mwingine.
Awali wakili wa wananchi hao Regold Nkya alisema kuwa wateja wake wanalalamikia utekelezaji wa Amri ya mahakama wa ekari 15 iliyotolewa na mahakama ya hakimu Mkazi Arusha ya kubomoa nyumba takribani 12 na leo wamekuja mahakamani hapo kutaka msaada zaidi wa kimahakama baada ya kukosa makazi ya kuishi
"Wateja wangu wanalalamikia utekelezaji wa amri ya Mahakama ya hakimu mkazi Arusha ,ambapo dalali wa mahakama Alan Mollel alitakiwa kukabidhi ekari 15 lakini katika hali ya kushangaza inaonekana dalali amekabidhi zaidi ya hapo na kuvunja takribani Nyumba 12 za wananchi hao kinyume na utaratibu"
Hata hivyo wakili Nkya alidai kuwa amewashauri wateja wake kukata rufaa lakini inavyoonekana hawapo tayari kufanya hivyo.
Ends......
0 Comments