RC NAWANDA AJINASUA NA KITANZI CHA KIFUNGO ,MAHAKAMA YAMWACHIA HURU

ByvNgilisho Tv-MWANZA



 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk.Yahaya Nawanda baada ya kupokea na kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili.


Akitoa hukumu hiyo baada ya kesi kusikilizwa kwa muda wa miezi minne Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Erick Marley amesema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamuhuri umeacha shaka katika maeneo mbalimbali hivyo kutomtia hatiani Dk.Nawanda.


Ametaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na video mjongeo 'CCTV footage' zilizowasilishwa kutokuonesha sehemu wawili hao walikuwa kwenye gari wakitenda tukio hilo.


Vilevile amesema sehemu nyingine iliyoacha shaka ni Jamuhuri kutokuwasilisha vipimo vya DNA vilivyochukuliwa kwa wawili hao.


Kadhalika amesema sehemu nyingine iliyoacha shaka ni maelezo ya shahidi namba mbili ambaye ni binti aliyedaiwa kulawitiwa.


Amesema kwenye ushahidi wake alidai kufanyiwa ukatili huo kwenye gari nyeupe lakini gari hilo haikuwa nyeupe bali ya silver.


Pia amesema binti huyo alisema wakati anafanyiwa kitendo hicho gari lilikuwa na vioo 'tinted' na nje hakukuwa na watu waliokuwa wanapita lakini video zilionesha gari hilo halikuwa na 'tinted' na pia watu waliokuwa wakipita nje na kuendelea na shughuli zao.

Post a Comment

0 Comments