PSSSF YAWANOA WASTAAFU WATARAJIWA ARUSHA, WATAHADHALISHWA NA MATAPELI,WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU YA FEDHA KWA KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

 Na Joseph Ngilisho,ARUSHA


KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha,Mussa Miseile amewashauri Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwa na nidhamu ya Matumizi ya fedha watakazozipata kwa kuwekeza katika miradi  waliyoizoea ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo.

Aidha aliwataka kujiepusha na matapeli ambao hutumia mbinu mbalimbali kuwarubuni wakijifanya wanania njema ya kuwaletea faida kwa kuzalisha fedha zao,jambo ambalo wengi wa wastaafu hujikuta wakiishia kutapeliwa.

Miseile aliyasema hayo leo NOVEMBA 17  Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wastaafu watarajiwa kwa wanachama wa PSSSF wa mkoani hapa na kuwasisitiza wastaafu hao watarajiwa  kuendelea kutunza Siri za serikali katika taasisi zao hata baada ya kukoma kwa utumishi wao.

"Tusipokuwa na nidhamu ya fedha na kutanguliza ulimbukeni wa aina yoyote baada ya kustaafu tutayafupisha maisha yetu , lazima tujifunze kuwa na nidhamu ya Matumizi ya fedha baada ya kuzipata kwa kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo ,pia epukeni matapeli"


"Epukeni uropokaji endeleeni kutunza Siri za serikali hata mtakapokuwa nje ya utumishi wa umma kutoa siri za serikali kunaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kuleta hatari kwa usalama wa taifa"

Katibu Tawala huyo aliwataka waajiri wote katika taasisi mbalimbali za umma kuhakikisha wanawasilisha michango ya watumishi wao kwenye mifuko ya uchangiaji ili kuondoa sintofahamu inayoweza kujitokeza baada ya kustaafu.

Awali  Mkurugenzi wa uendeshaji PSSSF ,Mbaruku Magawa Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa mfuko wa PSSSF miaka sita iliyopita jumla ya mafao ya thamani ya sh,Trilioni 10.46 yamelipwa kwa wanufaika wapatao 310 ,458.

Alisema mafunzo kwa wastaafu yanalenga kuwanufaisha katika maeneo ya uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo na vya kati ,uwekezaji katika masoko ya fedha ,kilimo biashara na ujasiriamali kwa ujumla 

Alisema katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2024/25 mfuko wa PSSSF unatarajia kulipa mafao ya uzeeni  lenye thamani ya sh, bilioni 560.79 wastaafu wapatao 11,622  na kulipa pensheni ya kila mwezi ya kiasi cha shilingi billion 980.33 kwa wanufaika 190,000 na kufanya mafao yatakayolipwa kwa Mwaka huu  wa fedha kiasi cha sh, Trilioni 1.54.

"Kupitia semina hii wastaafu wa PSSSF watatumia fursa ya kujifunza namna ya  kupanga maisha yao  baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa ya uwekezaji  wa mafao yao ili mafao hayo yaweze  kutoa mchango mkubwa katika fursa za kiuchumi"




Ends...




Post a Comment

0 Comments