MSHANA WA CHADEMA AMCHAKAZA SANARE WA CCM MURIET MASHARIKI ,ATAKA AKAGOMBEE KULEA FAMILIA YAKE AMESHINDWA KULETA MAENDELEO MIAKA MITANO, AJIBU MSHANA NI MTOTO MDOGO, NILIMCHAPA !

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA

WAKATI kampeni za UCHAGUZI wa serikali za Mitaa zikiendelea kutimua vumbi,mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema katika mtaa wa Mashariki  kata ya Murieth,jijini Arusha, Eliewaha Mshana amesema akichaguliwa atahakikisha anaziboresha barabara zote za mtaa huo ziweze kupitika kirahisi wakati wote wa msimu wa mvua.


Aidha mgombea huyo amemshangaa mgombea mwenzake wa ccm, Emanuel Sanare,kurejea kutetea  nafasi yake  wakati  hakuna  alichokifanya katika kipindi chote cha miaka mitano tangia achaguliwe na kumtaka abaki kuongoza familia yake kuliko kuendelea kuwadidimiza wananchi wa mtaa huo na hafai kuchaguliwa tena.


"Miongoni mwa mambo yaliyonisukuma kugombea nafasi hii ni mwenyekiti aliyekuwepo kutowashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo ya mtaa na kufanya mtaa huo kuwa na changamoto sugu ya  barabara mbovu"


Alisema changamoto zinazowakabili wananchi wa mtaa huo ni nyingi ambazo mwenyekiti aliyemaliza muda wake hakuwez kuzifanyia kazi ndio maana hadi leo wananchi wanateseka kwa ubovu wa barabara na hivyo ameamua kugombea ili  aweze kuzitatua kwa ari kubwa kwa kuwashirikisha wananchi.


Alidai kuwa Sanare tangia ameingia madarakani miaka mitano iliyopita hajawahi kutusomea mapato na matumizi,"tumekuwa na kiongozi ambaye hashirikishi wananchi kwa habari ya mapato na matumizi,hivyo kwa namna hiyo hafai kuwa kiongozi wa mtaa huo ni heri angabaki kuiongoza familia yake"


Akijibu Tuhuma hizo katika kampeni hizo zinazoendelea mtaani hapo, Mgombea wa CCM,Emanuel Sanare alieleza namna alivyojipanga kumalizia ahadi alizokuwa amebakiza katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.


Alisema hatishwi na mgombea huyo wa chadema kwani alishawahi kumwacha mbali katika chaguzi zilizopita hivyo hawazi kupoteza nafasi hiyo.


Akijibu hoja ya kutosoma mapato na matumizi ya mtaa huo alisema mgombea huyo hawezi kujua maendeleo ya mtaa huo kwa sababu sio mhudhuliaji mzuri wa mikutano ya maendeleo.


"Anachosema mgombea wa chadema ni uwongo kwa sababu sio mhudhuliaji wa mikutano ya maendeleo ya mtaa wa Mashariki, huyo mtu yupo kimaslahi binafsi na ni mtu mdogo sana tulishawahi kugombea naye huko nyuma nikamchapa vibaya sana "


Alisema wakati anagombea alikuta mtaa huo hauna nguzo hata moja ya umeme na kupitia uongozi wake alifanikisha wananchi wake kupata umeme.


Ends..


Post a Comment

0 Comments