MR MANGURUWE MZEE WA VANILLA AYAKANYAGA, AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UTAPELI,ASOMEWA MASHTAKA YA UTAKATISHAJI WA FEDHA HARAMU,AKOSA DHAMANA

By Ngilisho Tv-Dar Es Salaam

Mfanyabiashra wa Kitanzania, Simon Mkondya maarufu kama Dk Manguruwe (40) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 28 ikiwemo utakatishaji wa fedha wa Shilingi Milioni 90.



Manguruwe ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Vanilla International Ltd amefikishwa mahakamani na mwenzake Rweymamu Joh (59) ambaye ni Mkaguzi wa Kampuni hiyo.


Hata hivyo, wawili wamekosa dhamana kutokana na mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu kutokuwa na mamlaka ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19, huku washtakiwa wakipelekwa mahabusu.


Wawili hao wamesomewa mashtka yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya ambapo wanadaiwa walitenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Januari mosi mwaka 2020 na Disemba mosi mwaka 2023 ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.


Katika kesi hiyo ilidaiwa kwamba mashitaka 19 ni ya kufanya biashara ya upatu ,ambapo katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama  Mkurugenzi na John akiwa kama mfanyakazi wa kampuni hiyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kupata faida mara mbili hadi tatu kulingana ya kiasi cha fedha watakazotoa.


Ilidaiwa kwamba, washitakiwa hao walijipatia kiasi cha jumla ya sh milioni 92.2 kutoka kwa watu 19 tofauti ambapo watu hao walitoa kiato tofauti cha fedha ambapo aliwaahidi watapata faida mara mbili hadi tatu ya fedha walizotoa.


Iliendelea kudaiwa kwamba, mashitaka tisa ni ya utakatishaji yanayomkabili mshitakiwa Mkondya pekee ambapo kati ya Januari mosi mwaka 2020 na Desemba mosi 2023, akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni hiyo alijipatia jumla ya viwanja 9 kitalu namba AB  eneo la Idunda mkoani Njombe huku akijua viwanja hivyo ni mazalia ya makosa tangulizi ya upatu.


Baada ya kusomwa mashitaka hayo, Wakili Mrema alidai kutokana na mashitaka yanayowakabili, Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza hivyo washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote. 

Post a Comment

0 Comments