Na Joseph Ngilisho ARUSHA
VYUO vya Ufundi stadi hapa nchini vimetakiwa kufuata sheria kwa kuhakikisha vina usajili wa kisheria ,miundo mbinu iliyokaguliwa pamoja na kutumia mitaala inayotambulika na serikali .
Aidha vyuo hivyo vimetakiwa kutoa wahitimu bora wenye viwango vya kimataifa ili kukidhi soko la ushindani katika sekta ya utalii.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Vetà Kanda ya Kaskazini,Monica Mbele wakati wa mahafali ya 8 ya ngazi ya cheti katika chuo cha utalii cha Volcano kilichopo Sakina jijini Arusha ambapo jumla ya wahitimu wapatao 87 wa fani mbalimbali ikiwemo utalii,Mapishi,Ususi,Fundi Umeme na Magari walihitimu mafunzo ya Mwaka mmoja na kutunukiwa vyeti.
Mkurugenzi huyo mbali na kukipongeza chuo hicho kwa mahiri mkubwa namna kinavyotoa elimu na ujuzi, alisema jitihada zaidi zinahitajika kumudu ushindani katika sekta hiyo kwa kutoa wahitimu bora wenye viwango vya kimataifa.
Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka wanafunzi katika vyuo vya ufundi stadi vyenye usajiri kikiwemo chuo cha utalii cha Volcano na kuacha kuwapeleka watoto wao katika vyuo visivyoeleweka.
"Mahitaji ya mafunzo ya ufundi stadi hapa nchini ni makubwa sana na lengo la serikali ni kuhakikisha kila wilaya inakuwa na vyuo vya ufundi stadi ili kila mhitimu wa kidato cha anayetaka kujiendeleza anapata ujuzi aweze kujiajiri"
Aidha Mkurugenzi huyo alimwomba Mkurugenzi wa chuo hicho kuanzisha kozi fupi za kujifunzi lugha mbalimbali za kibiashara duniani ili kuwapatia fursa wanafunzi kupata ajira katika hoteli mbalimbali.
Alisema pamoja nachangamoto mbalimbali chuo hicho hakina budi kujikita kwenye ubunifu wa kimataifa ikiwemo kufundisha suala la Lugha za kimataifa ili kwendana na soko la ushindani duniani.
Aidha alitoa rai kwa wahitimu kuitumia elimu walioipata , kwenda kufanya ubunifu wenye tija na hadhi ya kimataifa ,namna ya kuanzisha na kuendesha biashara kwa kiwango cha tofauti kwa kujua wanalenga nini ili kukidhi mahitaji ya wateja wao .
Awali Mkuu chuo hicho ,Lazaro Thobias alisema chuo cha Volcano kimejikita kuzalisha wahitimu wenye viwango vya juu na wengi wa wahitimu zaidi ya asilimia 80 tayari wapo kwenye soko la ajira katika sekta mbalimbali mkoani hapa.
"Sisi chuo cha Volcano tunawaandaa vijana vizuri kwa kuwafundisha ujuzi unaoendana na teknolojia za kimaiaifa na wanaweza kufanya kazi popote duniani kwani tunawafundisha pia lugha mbalimbali za kibiashara za kimataifa"
"Vijana wetu katika soko la ajira tumewaandaa vizuri ambapo wanaweza kutumia kompyuta hivi sasa dunia imehamia kiganjani na tehama kwa ujumla"Alisema Thobias.
Alisema malengo ya chuo cha Volcano ni kupanua huduma zake na tayari wameanzisha ujenzi katika eneo barabara ya Bypass (EAC).
Naye diwani wa kata ya Eleray ,Losiaki Laizer alisema kuanzishwa kwa vyuo vya veta hapa nchini vinakwenda kutatua changamoto ya ajira hapa nchini.
Alisema mpango wa serikali wa ujenzi wa vyuo vya Veta ngazi ya wilaya umefanya vijana wengi wawe wajasiriamali waweze kujiajiri pale wanapohitimu kozi mbalimbali katika vyuo.
Ends....
0 Comments