MKURUGENZI HOSPITALI YA SELIAN AYAKANYAGA,ADAIWA KUMTWANGA MAKONDE NESS KUMFUNGIA STOO ,KUMTOMASA MAZIWA NA KUMTIMUA KAZI AOKOLEWA NA POLISI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA

MKURUGENZI wa Hospital ya Selian iliyopo Ngaramtoni wilayani Arumeru Mkoa wa ARUSHA,Amon Marti ameingia matatani akituhumiwa kuwanyanyaza kwa kipigo  na matusi wafanyakazi wake ikiwemo kumshushia kipigo mtumishi wa Hospital hiyo pamoja na kumtimua kazi bila kufuata taratibu.



Mmoja ya watumishi wa hospitali hiyo (jina limehifadhiwa),anayefanyakazi idara ya uangalizi wa watoto wenye ulemavu,alidai kunyanyaswa kingono na mkurugenzi huyo na Kisha kumshushia kipigo na baadaye kumfungia  stoo ya vifaa tiba kabla ya kuokolewa na polisi.


Alisema chanzo cha yeye kufanyiwa ukatili huo ni baada ya kutoa taarifa kwa mfadhili juu ya tukio la vifo vya watoto wawili ambao ni miongoni mwa watoto wenye ulemavu wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo chini ya Mradi wa mfadhili huyo.


 Alisema mkurugenzi huyo alichukizwa na hatua ya mtumishi huyo kutoa taarifa baada ya mfadhili kutembelea idara yake na kutaka kujua maendeleo ya watoto akihofia kukosa msaada wa fedha unaotolewa na mfadhili.


"Ilikuwa siku ya jumatatu wiki hii mkurugenzi alitangaza kunihitaji ofisini kwake ,nilienda katika kikao hicho na kukuta watu wengi sana alinihoji kwa ukali kwanini nimetoa taarifa ya vifo vya watoto kwa mfadhili,unataka mfadhili aondoke fedha zitapatikana wapi"??Alihoji 


"Mkurugenzi  huyo aliagiza niandikiwe barua ya kufukuzwa kazi na kunitaka  niondoke katika kikao hicho ,nikiondoka na kwenda ofisini kwangu na kuendelea na shughuli zangu wiki iliyofuata alinifuata ofisini na kunitukana sana na baadaye alianza kunipiga makofi na Kisha alinifungia ndani na kuondoka na funguo"


"Nikiwa peke yangu ofisini nimefungiwa nilichukua simu yangu na kuwapigia polisi kuomba msaada na polisi walipofika ,aliagiza  nifunguliwe na nikabidhiwe barua ya kufukuzwa kazi niondoke na nisionekane Tena hapo"


"Ni heri ni seme ukweli kuliko kukaa kimya waendelee kula fedha za marehemu ,unajua huyu mfadhili huwa anakuja na kutaka taarifa za maendeleo ya watoto na Mimi kama mkuu qa idara nampatia taarifa "


Alisema kabla ya tukio hilo Mkurugenzi  Dkt Mart alikuwa alinifuata ofisini mtumishi huyo na kumshikashika maziwa alimtaka kimapenzi ofisini huku alimwambia 'ukitaka hayo mambo yaishe kubali tumalize hapa hapa'


Alisema  Dkt Marti alishawahi kumwandikia barua ya kumfukuza kazi kabla ya wafanyakazi wenzake kulalamika na kutishia kumshtaki ndipo alipoagiza arejeshe kazini baada ya kukaa nje ya kazi miezi minne.


Mtumishi huyo ambaye amefanyakazi Selian  kwa zaidi ya miaka 15, ameiomba serikali kuingilia kati ili aweze kupata haki zake kwani wafanyakazi wanateseka sana na wameshangaa kuona mkurugenzi akifanya vituko kwa watumishi wake bila kuchukukiwa hatua yoyote na wamiliki wa hospitali hiyo ambao ni kanisa la KKKT.

Akihojiwa kwa njia ya simu dkt Amoni Marti alikana kumfahamu mtumishi huyo na kusema KUWA hakuna mtu aliyepigwa na kufukuzwa kazi katika hospitali hiyo.


"Mimi huyo mtu simfahamu nafikiri ni vizuri umhoji vizuri yeye mwenyewe na hapa hospitalini  hakuna shida yoyote na hakuna mfanyakazi wa namna hiyo Selian"Alisema Dkt Mart na Kukata simu bila kufafanua zaidi.


ends....





Post a Comment

0 Comments