WAPANGAJI AICC WACHARUKA WAMJIA JUU MKURUGENZI AICC NI BAADA YA KUWAPATIA NOTISI YA KUHAMA,BALOZI CCM NAYE AMCHARUKIA,TUKIPOTEZA WAPIGA KURA ATAJIBU,WAMTAKA WAZIRI MWENYE DHAMANA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

KITUO cha Mikutano cha Kimataifa AICC, Arusha kimeingia kwenye msuguano MKALI na wapangaji wake zaidi ya 400 baada ya Mkurugenzi wa Aicc Christina Mwakatobe kuwaandikia notisi ya kuwatimua katika nyumba za kituo hicho bila kuwashirikisha.

Wapangaji hao ambao baadhi yao wameishi katika nyumba hizo zilizopo Barabara ya Kijenge jijini Arusha kwa zaidi ya miaka 40 ,wamedai wameonewa na Mkurugenzi huyo ana maslahi yake binafsi na hawapo tayari kuondoka na wamejipanga  kumburuza  mahakamani Mkurugenzi wa kituo hicho kulalamikia utaratibu alioutumia wa kuwaondoa.


Akiongea kwa niaba ya wapangaji wenzake,Deepak Teja,alidai kwamba ameishi katika nyumba hizo kwa muda mrefu wa miaka 25 na Aicc imeshindwa kuwathmini wao kama wapangaji wa muda mrefu waliochangia mapato ya kituo hicho kwa kuamua kuwaandikia  notisi ya kuondoka bila hata kuwashirikisha.

"Tumepokea notisi kutoka aicc kwa masikitiko sisi kama wapangaji wa muda mrefu tuliochangia mapato ya serikali tulipaswa tushirikishwe lakini tumepewa barua ya muda mfupi ya kutakiwa kuondoka "

"Tunaomba tupatiwe walau miezi sita au mwaka kipindi hiki cha sikukuu tutapata wapi nyumba ya kuhamia na familia hizi "

"Sisi hatutaki kuondoka hizi nyumba ni nishani iliyoachwa na baba wa Taifa Mwl julias Nyerere ,kuna nyumba wamevunja kule Soweto mwaka 2012 na mpaka sasa hakuna mradi wowote uliofanyika huku aicc ikipata hasara kubwa ya kukosa mapato"

Naye balozi ya nyumba kumi katika eneo hilo ,Subira Mawenya alisema hatua ya aicc kukusudia kuwaondoa wapangaji wake ni kupoteza wapiga kura wa ccm ambao ni wapangaji wa eneo hilo.

Alisema chama kitakosa ushindi kwa kupoteza wapiga kura na kuitaka aicc isogeze mbele muda wa kuondoka kwa wapangaji wake walau miezi sita hadi mwaka kuliko notisi ya miezi mitatu na wengine miwili waliowapatia.

Jitihada za kumpata Mkurugenzi wa kituo cha  AICC ,Christine Mwakatobe ili kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wapangaji wake hazikufanikiwa licha ya kupigiwa simu  mara kadhaa na kupokea  lakini alikuwa akijibu yupo kwenye kikao mpaka majira ya usiku alikuwa akijibu hivyo,jitihads zaidi zinaendelea.

Wananchi hao wamedai hawapo tayari kuhama na wamemtaka waziri mwenye dhamana afike katika nyumba hizo ili kuzungumza nao na wapatia ufafanuzi.




Ends..





Post a Comment

0 Comments