LISU ALAANI KUKAMATWA KWA MBOWE ALITAKA JESHI LA POLISI WAKOME KUBUGHUDHI WAGOMBEA!

By Ngilisho Tv-MWANZA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amelaani na kukemea Jeshi la Polisi kumkamata Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe wakati akitekeleza majukumu yake ya kichama katika kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Lissu amekemea hatua hiyo jioni ya leo Novemba 22,2024 alipokuwa akihutubia wananchi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mabatini jijini Mwanza katika mwendelezo wa ziara ya kuwanadi wagombea wa uchaguzi wa serikali za mitaa kupitia chama hicho.


"Mchakato mzima  uliotumika kumkamata  Mbowe na viongozi wengine katika pori la Halungu lililopo wilayani Mbozi unarudisha nyuma mipango ya chama"


Katika hatua nyingine Lissu amewataka watanzania kushiriki kwa umoja katika uchaguzi huo kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho ili kusaidia kukabiliana na manyanyaso ya namna hiyo.



Post a Comment

0 Comments