JIJI LA ARUSHA LAONDOA ADHA YA WANAFUNZI KUCHANGISHWA KARATASI ZA MTIHANI, LAMWAGA 'RIM PAPER' 800 KWA SHULE ZOTE ZA SERIKALI NA BINAFSI,'MARUFUKU KUWACHANGISHA WANAFUNZI KARATASI ZA MTIHANI'-KAYOMBO

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imegawa karatasi za mitihani )Rim paper )800 kwa Shule za Msingi na Sekondari za serikali na binafsi katika Jiji hilo ikiwa ni mpango wa kuboresha elimu na  kuondokana na adha ya kuchangisha fedha kwa wanafunzi kwa ajili ya kununua karatasi hizo za mitihani.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kukabidhi kwa maboksi ya Karatasi hizo(Rims)Mkurugenzi wa jiji John Kayombo amesema halmashauri hiyo imeamua kulibeba jukumu hilo kwa lengo la kuwaondolea adha wazazi kuchangia karatasi za mitihani ya majaribio .

"Kuanzia sasa ni marufuku kuwachangisha fedha na kuwatuma karatasi wanafunzi, halmashauri imeamua kugawa karatazi hizo na kwamba suala hilo litakuwa endelevu"


 Aluongeza kuwa karatasi hizo  zitumike kwa shughuli iliyokusudiwa na kuahidi zoezi hilo kuwa la muendelezo kwa wakati wote atakapokuwepo katika utendaji wake katika  Jiji hilo.


“Ninaamini Walimu wote hawa ni waelewa na watazingatia maelekezo kama yalivyotolewa juu ya rim hizi, zoezi hili limefanyika kwa muda muafaka ambapo Wanafunzi wanaelekea kufanya mitihani ya kumaliza mwaka” ameeleza Kayombo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Shule za Jiji la Arusha Peter Pantaleo alisema msaada huo utasaidia kumpungizia mzazi gharama za michango ya ununuzi wa karatasi kwa ajili ya kufanyia mazoezi pamoja na mitihani mashuleni.


Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Msingi (TAPSHA) Halmashauri ya Jiji la Arusha Peter Malealle amesema” tunamshukuru Mkurugenzi wetu ametekeleza ahadi yake aliyoahidi mwezi uliopita ili kufanya elimu yetu kuwa na tija, na tunaahidi kutendea kazi” .


Aidha mwakilishi wa walimu Yusta Njau amempongeza Mkurugenzi kwa hatua hiyo ya kuwapunguzia wazazi mzigo na kuwataka wanafunzi kuongeza jitihada katika masomo yao ili kuunga mkono juhudi za Mkurugenzi katika kuboresha sekta ya elimu.






Ends..

Post a Comment

0 Comments