CHADEMA YAJIBU MAPIGO YAMWAMBIA KATIBU CCM AACHE PROPAGANDA,IMEJIPANGA KUPATA USHINDI MZITO SERIKALI ZA MITAA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimemjibu katibu Mkuu wa CCM Dr Emmanuel Nchini kwa kumwambia kuwa, kimejipanga kikamilifu kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kushinda na sio kweli kwamba chama hicho hakijawa tayari na uchaguzi huo kama ambavyo katibu huyo amesema.

Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu Mkuu wa chadema,Benson Kigaila wakati akiongea katika kikao cha uchaguzi jijini Arusha na  kusisitiza kwamba yeyote anayesema kuwa CHADEMA haikujiandaa kwa uchaguzi anapaswa kuwa na matatizo mawili  ama hakufuatilia mchakato wa maandalizi ya chama, au anafanya kazi ya ukuadi wa CCM kwa makusudi.


"Yeyote anayesema chadema hatukujiandaa na uchaguzi, awe Mwanachadema, awe MwanaCCM, awe hana Chama ana shida kati ya hizi mbili mosi, hakuwepo wakati wote wa zoezi hili hivyo hajui anachokizungumza au  anafanya kazi ya CCM kwa makusudi kabisa", alisema Kigaila.

Kwa ujumla, Kigaila anapinga vikali maoni ya katibu wa CCM,Emmanuel Nchimbi akionyesha wazi kwamba CHADEMA imejiandaa ipasavyo kwa uchaguzi na kwamba  kwa kusema hivyo anaonekana kuwa hana ufahamu wa hali halisi. 

Akitolea mfano baadhi ya majimbo, 'kwa mfano jimbo la  KAWE,lina mitaa 54 na chadema kabla ya kuanza zoezi la kuenguliwa kwa wagombea wetu, mitaa ambayo ilifanikiwa kuchukua fomu na kurejeshwa ilikuwa 51 sawa na asilimia 94 utasemaje kuwa Chadema ilikuwa haijajiandaa"

"Jimbo la Ubungo lina mitaa 46 waliofanikiwa kuchukua fomu na kurejesha kabla ya kuanza enguaengua ilikuwa ni mita 41,sawasawa na asilimia 87"

"Jimbo la Kibamba lina mitaa 44 na mitaa yote hiyo wagombea wetu walichukua fomu na kurejesha ,jimbo la ukonga lenye mitaa 70,waliochukua na kurejesha fomu ni mitaa 61,sawa na asilimia 87"

"Jimbo la Segerea lina mitaa 61 ,waliofanikiwa kuchukua na kurejesha fomu ni mitaa 60 sawa na asilimia 98,utasemaje kuwa chadema ilikuwa haijajiandaa"

Alisema  kanda ya Serengeti yenye mikoa ya Shinyanga ,Simiyu na Mara ina mitaa 420 na waliochukua fomu na kurejesha ni mitaa 378 sawa na  asilimia 99. 

Kigaila alimtaka dkt Nchimbi kuacha woga na siasa za Propaganda ,kwa kusema wapinzani hawajajiandaa "aache hayo maneno na mimi nisisitize kuwa chadema tumejiandaa na tutashiriki uchaguzi kikamilifu na tutashinda"Alisema 

Wakati huo huo hali ya sintofahamu imejitokeza katika uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Arusha, baada ya baadhi ya wanachama kuzusha vurugu
huku wakidai uchaguzi huo
umegubikwa na rushwa Pia, makada hao wamemtuhumu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, kuwapambania baadhi ya wagombea akitaka washinde.

wamemtuhumu Mwenyekiti
wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, kuwapambania baadhi ya wagombea akitaka washinde Hata hivyo, akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi leo Alhamisi Novemba 14, 2024, Lema amesema atazungumzia
suala hilo kwenye uchaguzi
wa viongozi Mkoa wa Manyara unaofanyika leo wilayani Babati.

"Unaweza ukatuma mwandishi wenu niko njiani ninakwenda Manyara kwenye uchaguzi nitatoa statement (taarifa) kwenye hotuba ya ufunguzi".
amesema Lema.

Wakizungumza usiku wa kuamkia leo Alhamisi Novemba 14, 2024, baadhi ya wanachama hao wamedai kufukuzwa kufuatilia uchaguzi huo na kuwa hawatakubali kuchaguliwa viongozi wasiowataka.

Akizungumza nje ya ukumbi uliokofanyika uchaguzi huo, mmoja wa wanachama wa Chadema Jimbo la Arusha, Boniface Kimario, alidai kuwa uchaguzi huo umeghubikwa na rushwa huku akidai Lema kupanga safi ya viongozi.

"Mnamtetea Lema nini, wanatuharibia hiki chama hamasa ninyi mnapewa maelekezo ya kuzima taa miaka yote, leo Lema hanijui mimi anaagiza niumizwe. kumshambulia mtu ni kosa, hamasa aliyenishambulia ameagizwa na Lema," amedai.

"Nimepigwa mateke nimeumizwa, hamasa aliyefanya hivyo ameagizwa na Lema huu uchaguzi umeanza asubuhi umeahirishwa kuna press (mkutano na waandishi wa habari), baada ya press kwa sababu wana malengo yao wameagiza taa zizimwe kwa sababu wana malengo yao,"
amedai.

"Huu ni uchaguzi wa mkoa
kila mtu ana haki ya kushiriki na kushuhuduia kiongozi wanayemtaka ni haki ya kila wmanachama, tumekuja wametuambia tutoke nje wakaridhika," amedai Boniface.


"Huu ukumbi tuna kumbukumbu nao ulizimwa taa kwenye uchaguzi wangu ulizimwa taa mara tatu matokeo yakabadilika. Leo (jana ) tumeenda kununua taa kuzuia hili jambo lisitokee, kuja na taa hapa Lema anaagiza hamasa wanitoe nje na nitawashitaki kwa majina yao," alidai.


Boniface alidai kipindi cha nyuma chaguzi kama hizo kulikuwa kunawekwa mpaka televisheni na ambao siyo wajumbe kama wao wanaangalia kinachoendelea ndani ila uchaguzi wa mwaka huu wamezuiwa na kufukuzwa.


"Huu siyo uchaguzi wenye kuzingatia demokrasia tumekubaliana na yote hayo, tunataka tuzuie taa isije ikazimwa bado Lema anaagiza tuumizwe na tupigwe, hiki chama kila mtu amedondosha jasho lake, kila mtu ametoa mchango wake kwenye hiki chama, wasiseme kuna kundi la wahuni, wote wanaogombea
wana sifa sawa". amedai.

"Huu uchaguzi umeghubikwa na rushwa ya kutosha, Lema amekuwa akipanga nani awe kiongozi lakini chama chenye katiba viongozi wanatokana na katiba siyo mtu,hatuwezi kusema CCM itoke madarakani halafu sisi hatuonyeshi mfano, uchaguzi unatakiwa kuwa huru na wa haki,' ameongeza.


Uchaguzi huo ulisimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, aliyekuwa akisaidiwa na Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa.

Akizungumzia tukio hilo, Golugwa amedai kuwa kuna watu wasiohusika ambao hawakuwa wajumbe hawawezi kuingia kwenye uchaguzi, kanuni zinataka wajumbe peke yao ndiyo wanaruhusiwa.

"Kuna watu kwa sababu ambazo hatukuwa tumezielewa waling'ang'ania kutaka kuingia kwenye uchaguzi, mfano uchaguzi wa wanawake wanaingia wanawake pekee, kuna baadhi ya wanaume walitaka kuingia kwenye uchaguzi wa wanawake pia kuna watu ambao kwenye mchujo walikatwa, kwa sababu za kikanuni baadhi yao waliendelea kubeba hisia".

"Kuna watu kwa sababu ambazo hatukuwa tumezielewa waling'ang'ania kutaka kuingia kwenye uchaguzi, mfano uchaguzi wa wanawake wanaingia wanawake pekee, kuna baadhi ya wanaume walitaka kuingia kwenye uchaguzi wa wanawake pia kuna watu ambao kwenye mchujo walikatwa, kwa sababu za kikanuni baadhi ya waliendelea kubeba hisia kuwa wanaonewa," amesema
Golugwa.


"Kwa mfano Baraza la Vijana linahitaji vijana kuanzia miaka 30 na usizidi miaka 35 kwenye uongozi, sasa mtu hana hicho kigezo Kilichofanyika ni kuwazuia wanachama wachache kwenye vyama hivi kuna watu wa kila namna hata wehu na wendawazimu tunao,wengine walikuja wamelewa,' amesema.


"Walizuiwa na walipotaka kutumia nguvu, nguvu zilitumika kuzuia, kwa hiyo walizuiwa hatuwezi kusema tumepigana. Huu ndiyo ufafanuzi halisi, dunia nzima kanuni za uchaguzi zinataka wajumbe pekee ndiyo waingie kwenye kikao, ni wendawazimu mtu anang'ang'ania awepo,”
ameongeza Golugwa.

Katibu huyo amedai kuwa baada ya wanachama hao kuondolewa, uchaguzi uliendelea vizuri na kumalizika kwa amani ambapo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mkoa ni Elisa Mungure, Katibu Viola Lazaro na Joyce Mukya kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha).


"Uchaguzi umeenda vizuri kwa amani, tumesimamia kwa haki bila shida, kwa hiyo hao wachache waliotengeneza drama ni wasumbufu tu ambao
kwenye vyama vyote huwa
wapo," amesema.


"Kuhusu wapigakura kutakiwa kupiga picha kura zao, wasifanye wanachama wote sisi wa Arusha na wasimamizi wa uchaguzi sisi ni wajinga hadi Lema akatuendesha, hapana.

"Hayo ni maneno ya kutunga hayo, watu wamepiga kura zao kwa siri hiyo Sh300,000 mtu
anatoa ya nini,?" alihoji.

"Tumechangishana pale hela ya chakula, ukumbi wote sasa hiyo Sh300,000 kwa kura moja huyo si mwendawazimu amerukwa na akili,uchaguzi tumesimamia kwa taratibu zote ikiwemo uhakiki wa wajumbe, kura zimepigwa za siri zikahesabiwa hadharani watu ndiyo wamechagua mtu wao,". amedai.

Golugwa amesema chama hicho kinatarajia kufanya uchaguzi wake wa viongozi Mkoa wa Manyara na baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa mkoa huo, utafanyika uchaguzi wa viongozi wa Kanda ya Kaskazini.



Ends..




Post a Comment

0 Comments