BOSS WA ANIF ALIYEFANYA MAPENZI NA WANAWAKE 400 WAKIWEMO WAKE WA VIONGOZI NA KUWAREKODI VIDEO AWAPONZA, RAIS ATANGAZA KUWATIMUA KAZI

By Ngilisho Tv-GUINEA

Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue amesema Serikali ya Nchi hiyo itawatimua kazini Maafisa na Watumishi wote wa Umma ambao ni miongoni mwa Wanawake zaidi ya 400 waliorekodiwa wakifanya mapenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha (ANIF) la Nchini humo, Baltasar Ebang Engonga (54) katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye Ofisi za Serikali na nyumbani kwa Ebang.


Ebang ambaye ni Baba wa Familia ya Watoto sita, tayari amekamatwa kwa kosa la kujirekodi akiwa anafanya mapenzi na Wanawake hao ambao wengine ni Wake za Watu Mdogo Mke wa Kaka yake, Binadamu yake, Dada wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mkuu wa Ulinzi wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Nchi hiyo na Mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Nchi hiyo.


Wengine walioonekana wakifanya mapenzi na Ebang kwenye video hizo ni Mke wa Mlinzi wake (Bodyguard), Mke wa Mchungaji wake, Wake wa Mawaziri kadhaa wa Nchi hiyo, Mke wa Mjomba wake ambaye ni Mjamzito, Marafiki 15 wa Mdogo wake wa kike na Wanawake wengine mbalimbali ambapo imeelezwa wote hao walionekana kuridhia video hizo kurekodiwa.


Ebang Engonga ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la ANIF ambalo ni Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha la Equtorial Guinea linalohusika na kusimamia uchunguzi wa kifedha na kusimamia shughuli zinazolenga kudhibiti ufisadi wa kifedha Nchini humo. 


MWAMBA Anasemaje yeye, msikie hapa!

Wanawake wengi waliniomba mimi niwarekodi hakuna aliyelazimishwa wale ni watu wazima hakunq mtoto mdogo pale 
Kwani wengine walienda na kurudi tufanye tena hivyo tumekuwa tukifurahia 

 Afya yangu ni njemq kabisa nitashangaa kusikia kuna mwanamke ana maambukizi hilo sio kweli.

Jambo naloweza kuwambia Wanaume wenzagu ni kuangalia namna bora ya kuishi katika dunia hii hasa wawapo na wake zao unaweza kuniona mimi mkosaji ila nimeonesha dunia kuwa mwanamke ni kiumbe cha namna gani kuliko kunihukumu kaa tafakari na jifunze kuhusu wanawake .

Amefunguka mwamba

Post a Comment

0 Comments