ARUSHA: MGOMBEA WA CCM MTAA WA KIRIKA B AMTWANGA MAKONDE DIWANI WAKE AKIDAI AMEKATA JINA LAKE,KESI YATUA POLISI ,POLISI LAWAMANI KWA KUFUMBIA MACHO, DIWANI AJERUHIWA VIBAYA KWA KUPIGWA NA CHUPA YA BIA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA


Mgombea wa chama cha Mapinduzi CCM  mtaa wa Kirika B Kata ya OSUNYAI jijini Arusha,Shaban Mohamed,anadaiwa kumtwanga makonde mazito diwani wa kata hiyo Christopher  Rupagwelela akimtuhumu kuhusika kukatwa jina lake.


Shaban ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa huo aliyemaliza muda wake alichuku fomu kutetea nafasi yake lakini aliingiwa na mfadhaiko wa akili baada ya kusikia jina lake limekatwa na kuamua kutenda tukio hilo akimhisi  diwani huyo ndiye aliyehusika kukatwa kwa jina lake jambo ambalo diwani huyo amekana kuhusika.

"Kikao cha halmashauri ya wilaya ina watu zaidi ya 100 mimi haweza kuhusikaje kukata jina la mgombea "??alihoji diwani huyobwakati akihojiwa na mwandishi wa habari.

Christopher alisema kuwa wakati anatoka kwenye kikao cha Halmashauri ya wilaya kilichoketi kwa ajili ya kuchuja majina ya wagombea,majira ya  usiku alipita mahala kwa lengo la kunywa soda na baadaye shaban alifika eneo hilo na kuanza kumshambulia diwani huyo kwa matusi akidai amekata jina lake.

"Awali niliona Shabani kama amelewa niliamua kuondoka kuelekea nyumbani kwangu na nilipofika karibu na ukuta wa nyumba yangu majira ya saa saba usiku nilishangaa kumwona shaban akiwa amejibanza kwenye ukuta kando na geti langu la kuingilia na ghafla alinirukia akiwa na chupa mkononi akitaka kunidhulu ,nikifanikiwa kumshika na baadaye  majirani walitokea na kutuamua"

Alisema baadaye alienda kutoa taarifa kituoni cha polisi  kwa ajili ya hatua zaidi ila anashangaa hadi sasa mtuhumiwa hajakamatwa ama kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa ili kujua nia yake ya kumshambulia.

Diwani alisisitiza kuwa hahusiki na madai ya Shaban kwani kikao cha kuchuja majina ya wagombea ndani ya chama kina taratibu zake na  maamuzi hutokewa na wengi na siyo yeye peke yaKe.

Naye balozi wa mtaa huo,Daniel Loshie alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa diwani aliumia kwenye kichwa na kupata majereha ya mguu na mkono.

Akizungumzia mkasa huo,balozi Loishie alisema kuwa Shabani ndio alimshambulia diwani kwa matusi na baadaye alimfuata nyumbani kwake kumvuzia akiwa na chupa ya bia mkononi akiwa na lengo la kumdhulu.

"Kuna mahala tulikuwa tumekaa tukiwa na Shaban na alisikika akiniambia kuwa anataka ampige huyo mzee(diwani)nilimhoji kwanini, aliniambia amekata jina langu nilimwambia usifanye hivyo" 

"Baada ya muda alikuja Shaban na kuanza kumtukana diwani na baadaye alimfuata nyumbani kwake usiku na kumvizia kwenye ukuta wa nyumba akiwa na chupa ya bia mkononi ,diwani alipofika shabani alimrukia ndipo walishikana na kuanza kuzichapa"

Jitihada za kumpata shaban Mohamed ili kuzungumzia madai hayo hazikuwez kuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa na alipotumiwa ujumbe wa simu alijibu atanitafuta kwa mazungumzo zaidi.

Ends..






Post a Comment

0 Comments