Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Mkoa wa utalii Arusha imeandaa maonesho ya kwanza ya kutangaza Utalii wa Zanzibar yatakayowakutanisha wawekezaji ,watalii na wadau wa sekta mbalimbali kutoka ndani na Nje ya nchi.
Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha leo OKTOBA 5 ,2024 ,Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Arif Abbas Manji,alisema maonesho hayo yatafanyika oktoba 25 na 26 mwaka huu katika kituo cha Maonesho cha Zanzibar,Dimani yatakayoshirikisha pia wadau wa utalii zaidi ya 250.
Kupitia katika Maonesho ya kwanza ya Tamasha hilo la Utalii na Uwekezaji , Zanzibar inatazamiwa kutumia kikamilifu fursa hiyo kuonesha namna inavyoimarisha Mazingira ya Uwekezaji na kukuza Sekta ya Utalii kama sehemu muhimu ya kukuza Uchumi wake.
Akiwa Jijini Arusha kwa ajili ya utambulisho wa ujio wa maonyesho hayo Manji alisema hiyo ni fursa ya pekee kwa Zanzibar kuonesha fursa zilizopo akitaja ushirikiano kati ya Visiwa hivyo na Mkoa wa Arusha kuwa turufu muhimu ya kuongeza tija katika kukuza sekta ya utalii kupitia utangazaji wa vivutio vya Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema Kamisheni ya Utalii Zanzibar ina vipaumbele vitano vikuu katika kuimarisha na kutangaza utalii wa Zanzibar ambayo ni pamoja na Utalii wa Uruthi,Utalii wa Michezo,Utalii wa Afya,Utalii wa Halal na Utalii wa Mikutano na Maonesho (MICHE)
"Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kupitia Kamisheni ya Utalii inatangaza rasmi Maonesho ya kwanza ya Utalii na uwekezaji Zanzibar yatakayofanyika Oktoba 25 -26 Mwaka huu yakiwa na kauli mbiu ,kukuza Utalii Endelevu ,Uhifadhi wa urithi na uwekezaji "Alisema Manji.
Alisema kuwa uchumi wa Zanzibar umekuwa ukipitia Mabadiliko Makubwa ,ambapo sekta ya utalii ikiwa ndo sekta mama inayochangia zaidi ya asilimia 30 ya pato la Taifa (FDP) na asilimia 80 ya fedha za kigeni. Ongezeko la wageni limefikia 638,498 sawa na asilikia 16.4 zaidi ya mwaka 2022.
"Maonesho hayo ya utalii Zanzibar 2024 yatashirikisha wadau Zaidi ya 250 ikiwa ni pamoja na wamiliki wa Hotel,vivutio vya Utalii ,waongoza watalii na wawekezaji ambapo watapata fursa ya kushiriki semina za kipekee zinazolenga kutoa maarifa hususani fursa za uwekezaji na maendeleo katika utalii wa Zanzibar "Alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda akizungumza baada ya kupokea ujumbe huo kutoka kamisheni ya Utalii Zanzibar amepongeza hatua hiyo na kueleza kuwa ni mwanzo mzuri wa ushirikiano kati ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mkoa wa Arusha katika sekta ya utalii.
Makonda ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar namna inavyopambana kukuza sekta ya utalii kupitia vivutio vyake vya asili pamoja na ubunifu walioufanya wa kuandaa onesho hilo la kipekee na la kwanza.
"Niwaombe wadau wa utalii kutoka hapa Arusha muweze kuhudhulia maonesho hayo yanayoambatana na semina ya utalii ilinkukuza sekta ya utalii Zanzibar na Tanzania bara na mimi natamani sana Arusha na Zanzibar tuwe mapacha tuweze kuuza kwa pamoja bidhaa zetu kwenye soko la dunia"Alisema.
Makonda pia amegusia ujio wa onesho lake Kubwa la Magari aina ya LAND ROVER linalotazamiwa kufanyika Mkoani hapa kuanzia Octoba 12 hadi 14 Mwaka huu magari ya aina hiyo zaidi ya 1000 yakitazamiwa kushiriki kutoka nchi saba hadi tisa afrika ambazo zimethibitisha kushiriki katika viwanja vya magereza jijini Arusha.
Aidha alisema onesho hilo pamoja na mambo mengine linalenga kuvunja rekodi ya Dunia ya maonesho ya Magari hayo ambalo iliwekwa na Taifa la Ujerumani kuwa na magari hayo yaliyofikia urefu wa kilometa saba na sasa rekodi inatarajia kufikia kilometa 12.
Ens...
0 Comments