WATU WANNE WAFARIKI DUNIA,15 WAKIJERUHIWA KATIKA BASI LA KAPRIPON

By Ngilisho Tv -TANGA


WATU wanne wamekufa na wengine 15 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Kapricon (T 605 DJR) iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha kupata ajali na kupinduka katika eneo la Maili Kumi, barabara ya Segera-Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imetokea ya saa 7:30 usiku, ambapo basi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Julias Mushi,43, mkazi wa Arusha


Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa madereva kufuata sheria za barabarani nyakati zote ikiwemo kuchukua tahadhari kuepuka madhara ambayo yangeweza kuepukia.


Post a Comment

0 Comments