Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Arusha Mjini,John Kayombo ameongoza mamia ya wakazi wa jimbo hilo kujiandikisha daftari la Mpiga kura katika kituo cha shule ya sekondari Olorien na kuwahimiza wananchi ambao bado kutumia fursa hiyo ili kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27 Mwaka huu.
Akiwa katika kituo hicho alieleza namna zoezi hilo linavyoendelea vizuri na kwamba katika vituo 40 alivyotembela hakuna changamoto wala malalamiko yoyote yaliyojitokeza.
Kayombo ambaye pia ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha, aliwataka mawakala wa vyama vya siasa ambao hawakupata kursa ya kula kiapo kwa wakati ,ametenga chumba maalumu cha kuwaapisha ofisini kwake na kuwataka kwenda kula viapo ili kushiriki ziezi hilo kwa uaminifu.
Mwandikishaji katika kituo cha Moivoi kata ya Olorien, Rose Mkundi alisema katika kituo chake zoezi linaenda vizuri na mwitikio ni mkubwa.
"Tangu tumefungua kituo mwitikio ni mzuri na watu wanaendelea kujiandikisha kwa wingi"
Mmoja ya wananchi Vedeus Masawe mkazi wa Moivoi alipongeza utaratibu iliotumika katika kujiandikisha kwani wananchi wanachukua muda mfupi wa dakika tatu kujiandikisha na kwenda kwenye majukumu yao.
"Utaratibu uliotumika umesaidia sana watu kutokaa kwenye vituo kwa muda mrefu na kutumia muda mfupi ,mimi nimetumia dakika tatu na kuondoka"
Alisema suala la kujiandikisha ni jambo la msingi sana litakalo mwezesha mwananchi kutumia haki yake ya msingi kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowahitaji.
Zoezi hilo la kujiandikisha limeanza leo Oktoba 11 hadi oktoba 20 Mwaka huu majira ya saa mbili hadi saa 10 jioni.
Ends..
0 Comments