Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia wanandoa wawili ,Jaina Mchomvu(50) na Ramji Hatibu Mlacha(60) wakituhumiwa kumuua kwa kumchinja mwanafunzi wa darasa la Sita wa shule ya Msingi Domino, Mariam Juma(12) mkazi wa kwa Mrombo katika jiji la Arusha
Jaina Mchomvu,mtuhuniwa wa mauajiMtoto Mariam Juma, hatunaye!
Tukio hilo la kusikitisha linalohusishwa na imani za ushirikina,mwili wa marehemu ulikutwa mchana saa sita chini ya uvungu wa kitanda ukiwa umekatwakatwa vipande na kuwekwa kwenye beseni baada ya mjukuu wa mtuhumiwa kuona mkono wa marehemu ukining'inia wakati akitafuta kiatu .
Kamanda Masejo alisema hadi sasa watu watatu wanashikiliwa akiwemo mshukiwa namba moja Jaina Mchomvu ambaye amekamatwa na askari Polisi huko Mabogini Moshi, Mkoani Kilimanjaro alikokimbilia kujificha baada ya kutenda tukio hilo.
SACP Masejo alisema kuwa Baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa, Jaina Mchomvu alihojiwa na kukiri kutenda tukio hilo la mauaji ya mtoto huyo.
Alifafanua kuwa Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za kiuchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kwamba Mwanamke huyo ambaye anaishi jirani na wazazi wa marehemu ,alikuwa muumini wa Swala Tano wa dini ya kiislamu amekuwa akiishi na mume wake aitwaye ,Hatibu Mlacha lakini siku ya tukio aliondoka kusikojulikana na alimpigia simu mtoto wake wa kike aitwaye Ramji na kumwagiza aende nyumbani kwake kumsaidia kufua.
Taarifa zimedai kuwa Ramji alifika nyumbani kwa mtuhumiwa(Mama yake) akiwa na mtoto wake na wakati akiendelea na shughuli za usafi ghafla mtoto wake aliyekuwa akitafuta kiatu chini ya uvungu alimwambia ameona mkono wa mtu chini ya uvungu kwenye beseni.
Ramji ambaye pia anashikiliwa na polisi aliingia ndani na kushuhudia mkono wa mtu na kuanza kupiga kelele ndipo wananchi walipojitokeza na baadaye polisi walifika eneo la tukio na kuondoka na mwili wa marehemu.
Hata hivyo taarifa zinadai kuwa huenda mtuhumiwa anamtandao uhaohusishwa na mauaji ya watu wengi zaidi kutokana na karatasi mbalimbali zilizokutwa nyumbani kwake zimeandikwa orodha ya watu waliouawa.
Polisi katika kituo cha Muriet walifika nyumbani kwa mtuhumiwa wakiwa wameambatana naye kwa lengo la kumpekua baada kufanikiwa kumtia mbaroni na kuondoka na nyaraka mbalimbali likiwemo sanduku kubwa linalodaiwa kuficha viungo vya binadamu.
Katika hatua nyingine wananchi wenye hasira kali wamebomoa nyumba yote ya mtuhumiwa na kuisambaratisha na kisha kuteketeza kwa moto vitu mbalimbali zikiwemo nguo huku baadhi ya vitu vyake vikiporwa.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa leo baada ya kukamilika shughuli za kiuchunguzi.
Ends.
0 Comments