RC MAKONDA HATAKI MCHEZO AMCHAPA KIAINA GAMBO AZUNGUMZIA ANAVYOTOFAUTIANA NA VIONGOZI WENZAKE HASA MADIWANI KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO,AGUSIA MAJUNGU UNAFIKI NA USHIRIKINA,AMPA MENO YA KUNG'ATA MEYA WA ARUSHA, WAZIRI MCHENGERWA ATAKA MAKONDA AENDELEE 'KUPIGA SPANA'

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Mkuu wa Mkoa Arusha ,Paul Makonda amewashukia vikali baadhi ya viongozi katika jiji hilo ambao wamekuwa  wakitofautiana kwenye  shughuli za  maendeleo kwa maslahi yao binafsi kwa kuendekeza chuki,fitina na ushirikina huku ikionesha wazi kumlenga mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo.

Akiongea kwenye mkutano wa hadhara wa waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa katika viwanja vya Kilombero jijini hapa,Makonda ambaye anazaidi ya miezi sita Tangia apate uteuzi wa ukuu wa Mkoa huo,alisema hafurahishwi na baadhi ya viongozi kutokuwa na mahusiano mazuri na viongozi wenzao.

"Nilichogundua Tangia nimeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huu ni baadhi ya viongozi wenu kutokuwa na mahusiano mazuri na viongozi wenzao akiomba jambo hapewi,kuendekeza siasa za Majungu ,kiasi kwamba ukiendekeza majungu ,mahusiano mabovu, ukachanganya na ushirikina mtapata barabara kweli hapo"??alihoji Makonda huku akishangiliwa kwa nguvu sana na wananchi.

"Unakuta ,kutwa viongozi wanatengenezeana ajali ,kutwa majungu ,shoti za kutosha hamuwezi kupata maendeleo lakini nimemwambia waziri wangu Mchengerwa Meya huyu wa jiji na wenyeviti nimekaa nao vikao nataka wawe na mamlaka kamili kama ambavyo sheria imetutaka tuwawezeshe  serikali za mitaa"

Alisema "Meya na madiwani kwa kushirikiana na mbunge ndio wawakilishi wa wananchi lakini utakuta wakikaa kwenye vikao vyao wakiamua anatokea mtu moja anasema mlichokiamua hakifanyiki"

"Sasa mimi nime sema huu mkoa ni mwingine Naingia vitani mwenyewe nikiona mtu anamnyanyasa diwani ama Meya staki mtu achanganywe utakuta hata Meya hajiamini ,namimi nimekaa nao vikao na kuwaambia teteeni maslahi ya  wananchi "

Aliwataka madiwani kuwa wakali ili kukomesha wizi wa fedha kwenye halmashauri alisema alipoteuliwa alikuta sh, milioni 20 za jiji zinarudishwa serikali kuu wakati watu hawana matundu ya vyoo ,watu hawana madarasa barabara mbovu lakini wamekalia majungu ushirikina na siasa uchwara"

Katika hatua ngingine Makonda alilazimika kuondoka kwenye kiti chake na kwenda kumtaka gambo apishe eneo alilokuwa ameketi ili kumpisha  Meya wa jiji la Arusha Maxmilian Iranghe akaye ambaye alionekana kukaa pembeni mwa viti vya meza kuu na kukosa mawasiliano ya karibu na waziri Mchengerwa!

Awali Gambo akiongea katika mkutano huo baada ya kupata fursa hiyo , alimshukuru Rais Samia Suluhu kwa fedha nyingi alizozielekeza katika jiji la Arusha ikiwemo mradi wa  uwanja wa mpira unaojengwa kwa thamani ya sh,bilioni 286.

Pia alisema Rais samia ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule Tano za mfano ,ujenzi ya barabara, miradi ambayo inagharimu fedha nyingi zilizotolewa na serikali.

"Mh waziri ulitoa maelekezo kwa halmashauri zote nchi nzima lazima zitenge fedha kutoka mapato yake ya ndani kw ajili ya ujenzi wa barabara na sisi katika halmashauri yetu tumetenga sh bilioni 2.1 na leo nakushukuru sana umetoa maelekezo kwa Tarura kufuatilia hizo fedha ili kuanza ujenzi wa barabara ya Esso hadi Longdon kwa ajili ya kuanz ujenzi kwa kiwango cha Lami"

Kwa upande wake waziri Mchengerwa ,alimpongeza mkuu wa mkoa Makonda kwa kazi nzuri anayoifanya katika kipindi kifupi alichohuduma baada ya kuteuliwa kutokana na kasi yake ya maendeleo na ubunifu wake.

"Nataka niwambie Makonda chapa kazi asikubabaishe mtu yoyote hapa kazi ulioifanya kwa wananchi wa Arusha inaonekana kwa macho unashugulika na maskini ,unashughulika na yatima ,unashughulika na wajane hii ndo kazi rais samia aliyokutuma chapa kazi endelea kupiga spana rais Samia anakuamiani sana"







Ends..




Post a Comment

0 Comments