RAIS SAMIA AKABISHI ENEO LA KANISA KATOLIKI KWA BABA ASKOFU, LILIKALIWA KIBABE , POLISI TRAFIKI WAJIPANGE KUTAFUTA PAKWENDA ,ASKOFU AMANI ASHUSHA NONDO ,ALAANI UBABE,ULAFI NA CHUKI BINAFSI.

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Rais Samia Suluhu Hassan amemaliza mgogoro wa muda mrefu baina ya kanisa na halmashauri ya jiji la Arusha uliodumu kwa miaka 30 baada ya kuamuru kurejeshwa kwa Eneo la kanisa katoliki jijini Arusha lenye ukubwa wa takribani mita za Mraba 7503 lililokuwa limepokonywa na halmashauri  ya jiji hilo.

Akikabidhi eneo hilo lililopo karibu na kituo cha polisi Trafiki jijini Arusha kwa niaba ya rais Samia ,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul  Makonda aliyekuwa ameambatana na Mkurugenzi wa jiji la Arusha, John kayombo pamoja na meya wa jiji Maxmilian Iranghe, amesema hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Mgogoro huo kumfikia Rais  Samia na kumwagiza Waziri wa TAMISEMI,Mohamed Mchengerwa kulikabidhi eneo hilo kwa Kanisa Katoliki jimbo kuu la Arusha bila mashari yoyote.

Aidha aliagiza kurejeshwa kwa fedha kiasi cha sh,milioni 500 ambazo kanisa lilikuwa limezilipa kwa lengo la kukomboa eneo lao baada ya halmashauri ya jiji la Arusha kuwataka wafanye hivyo .

Makonda alisema Serikali ililichukua eneo hilo kwa matumizi yake na kisha baadae kulitaka Kanisa hilo kutoa Milioni 500 za kulipia eneo hilo wakati kanisa lilipoanza mpango wake wa kuongeza eneo la utoaji wa huduma mbalimbali kanisani hapo.

Kwa Upande wake Mhashamu Baba Askofu Dkt. Isaac Amani, Askofu wa Jimbo kuu Katoliki  Arusha, amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwa mtatuzi wa changamoto mbalimbali za wananchi huku pia akikemea Ubinafsi, Ubabe, Kutojali maendeleo ya wengine pamoja na Ulafi kwa baadhi ya watumishi wa Umma wasiokuwa waaminifu nchini .

"Namshukuru mungu sana leo tumeona kama miujiza kwa muda mrefu wa takribani miaka 30 tumekuwa tukifuatilia eneo letu tumeshaandika sana barua hatimaye siku ya mungu imefika na leo tumekabidhiwa eneo letu"


"Tulikuwa tukifuatilia manispaa baadaye tukaambiwa tulipe sh, milioni 500 ili kuhamishwa shule iliyokuwa katika eneo letu tuliona wanafunzi wamehamishwa tukalipa sh, milioni 500 ili tukabidhiwe ila hatukukabidhiwa hadi rais samia alipoingilia kati na leo tumekabishiwa eneo letu".

Alisema  kiasi cha sh, milioni 500 walizokuwa wamechanga na kuilipa  halmashauri kwa lengo la kukomboa eneo lao wamerejeshewa na sasa kanisa lina amani na wamejipanga kulitumia eneo hilo kwa ajili ya maendeleo mapana ya kanisa.






Ends..


Post a Comment

0 Comments