By Ngilisho Tv Dodoma
Baraza la Maadili limemaliza kumhoji Mkuu wa Chuo cha uhasibu (IAA )Arusha,Professa Eliamani Sedoyeka kuhusu tuhuma nne zinazomkabili ambapo katika majibu yake amedai hazina ukweli wowote na kwamba alifuata taratibu zote za kiutumishi katika kufanya maamuzi .
Akijibu Tuhuma ya kuwa na ukaribu na mtumishi Hakimu Ndatama na uhamisho wake kurudi IAA pindi yeye aliporejea kuwa Mkuu wa Chuo Prof amesema kwamba Uhamisho wa Ndatama kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ulifuata taratibu zote za kisheria na kufuatia mahitaji ya kikazi, Chuoni hapo na hakuna ukiukwaji wowote .
Alieleza kwamba Chuo kiliandika Barua kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba,Ndatama arejeshwe.Zoezi hilo lilifanyika kabla ya yeye kurejeshwe Chuoni IAA hapo kutokana na mahitaji ya kikazi .
Na kuhusu Tuhuma za Uteuzi wa Hakimu Ndatama kuwa Mkuu wa Kitengo, Sedoyeka alieleza kwamba Kuhusu tuhuma ya kutekeleza uteuzi wa Hakimu Ndatama na mgongano wa maslahi, napenda kueleza kuwa uteuzi huu ulikuwa na msingi mzuri unaozingatia uwezo na ufanisi wake katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi chuoni hapo .
Alisema kwamba alizingatia sifa za Ndatama na uwezo wake wa kuchangia maendeleo ya IAA akiwa na dhamira ya kulinda maslahi ya taasisi na kuhakikisha kwamba wanapata watu wenye uwezo na wivu wa kuchangia maendeleo katika kufikia malengo ya taasisi.
Alifafanua kwamba Ndatama si ndugu yake wala si kabila lake wala hakuna chochote kinacho muunganisha nacho na kuwa na maslahi juu yake.
Kuhusu malalamiko juu ya Zabuni ya Viti na Meza vya Wanafunzi kwa Kampasi ya Babati Professa alisema kwamba Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na. 7 ya mwaka 2013), inampa mamlaka Afisa Masuuli kukataa kuendelea na zabuni ama kurejesha zabuni kwenye Bodi ya Zabuni.
"Ninaweka wazi msimamo wangu kwamba nilifuata taratibu zote na sikuvunja sheria bali nilikuwa nikitekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa Sheria"alisema na Kuongeza
"Kama kiongozi mwaminifu kwa nchi yangu, nimekuwa makini kuhakikisha taasisi inapata bidhaa bora kwa njia za uwazi na kwa gharama nafuu kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma".
Na kuhusu Tuhuma za Uhamisho wa Ndani wa Mtumishi Robert Mwitango alieleleza kwamba Kwa ujumla uhamisho wa ndani wa watumishi hufanywa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kiutendaji wa taasisi.
Katika Mwaka wa 2023/2024 Idara ya Maktaba ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo zile ambazo kwa uhalisia wake zilihitaji
msaada wa karibu wa kitengo cha Manunuzi ya Umma, kama Stock taking, Asset Verification” na Ununuzi mkubwa wa vitabu kwa mkupuo.
Awali prof. Sedoyeka, Oktoba 16,2024 alifikishwa mbele ya Baraza la Maadili kwa malalamiko Manne ya kukiuka maadili ya viongozi wa umma.
Malalamiko hayo ni kumpandisha cheo mtumishi kwa upendeleo, kuingilia mchakato wa ununuzi wa viti na meza, kuwa na uhusiano wa karibu na mtumishi na kufanya uhamisho wa ndani wa mtumishi kinyume na maadili ya viongozi wa umma.
Ends...
0 Comments