NABII NAMBA SABA GENERALI WA UPAKO HAKAMATIKI BAADA YA UKIMYA MREFU AZINDUA BONGE LA KANISA HATARIIII,MAASKOFU NA WACHUNGAJI KUTOKA MAKANISA RAFIKI WAMIMINIKA KAMA MVUA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Nabii namba Saba Maarufu kama General wa Upako amezindua makao makuu ya kanisa la KINGDOM OF GOD katika eneo la Lekamba wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha ikiwa ni mpango wake wa kupanua huduma  na kuwasogezea karibu huduma ya kiroho wakazi wa eneo hilo ambao kwa muda mrefu wamekuwa na kiu ya kupata huduma ya kiroho.

Katika uzinduzi huo ulioenda sanjari na kusimikwa kwa wachungaji zaidi ya 40 kutoka madhehebu mbalimbali ya kikristo,Nabii namba saba alisema ndoto ya kueneza neno la mungu kwa wakazi wa Maeneo ya pembezoni imetimia na itasaidia kupunguza matukio yasiofaa kwa baadhi ya wananchi.

Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya waumini ,wachungaji na  Maaskofu kutoka madhehebu rafiki ndani na nje ya nchi alisema  anamshukuru sana mungu kwa kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo katika eneo lenye ukubwa wa ekari tatu ambapo atakidhi kiu ya wananchi katika kuabudu.

Nabii namba Saba alisema awali alikuwa akitoa huduma hiyo ya neno na maombi katika kanisa hilo lililokuwa eneo la kukodisha la ,Ngaramtoni lakini anamshukuru mungu baada ya kukamilika kwa ndoto yake ya kujenga makao makuu kanisa hilo lenye matawi mbalimbali hapa nchini.

Kanisa hilo ambalo lipo umbali wa kilometa 7 kutoka barabara ya Lami  Kisongo ,waumini wake wanaweza kufika kwa magari ya Haice yatakayokuwa yanawaleta waumini hao na kuwarejesha .





"Awali tulikuwa tukitoa huduma ya neno na maombi katija eneo la kukodisha hapo Ngaramtoni , lakini tulifika mahala tukaona haina haja ya kukodisha ni heri tupate eneo la kujenga makao makuu yetu na leo maono yetu yametimia "

Alisema ujenzi wa kanisa hilo umesaidia kuwasogezea huduma wananchi wa eneo hilo kama Umeme,maji na wanampango wa kuboresha barabara inayoelekea katika eneo hilo la huduma ili iwe kwa kiwango cha changarawe.

Naye mmoja ya Maaskofu waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi na kusimikwa kwa wachungaji 40  ,Askofu Philemon Mollel wa kanisa la KKAM  ,alimpongeza Nabii namba saba kwa hatua ya kuboresha huduma yake na kujenga makao makuu ya kanisa hilo.

"Hiki alichokifanya nabii namba saba cha kuimarisha makao makuu ya kanisa na kuwainua watumishi zaidi ya 40 kwa kuwawekea mikono ni jambo jema sana na sisi  kama viongozi wa dini tumekuja kumtia shime ili kuendelea kueneza kazi ya mungu "alisema Askofu Mollel.





Ends...




Post a Comment

0 Comments