MASKINI! MFANYABIASHARA MZITO WA MADINI ARUSHA AUAWA KINYAMA MWILI WAKE WAKUTWA UKINING'INIA KWENYE MTI WA MLIMA WA MAOMBI,WAUAJI WAPIGA SIMU KWA NDUGU ZAKE KABLA YA KUTEKELEZA TUKIO HILO

Na Joseph Ngilisho-ARUSHA 

Mfanyabiashara  wa madini ya ujenzi(Moramu), David Mollel  mkazi wa Kata ya Moivaro, ameyawa na Watu wasiojulikana na mwili wake kuning'inizwa kwenye mti  juu ya Mlima Oldonyowas, jirani na  eneo linalotumika kwa maombi .


Inadaiwa Mollel mwenye umri wa  kati ya miaka 50 na 55, aliuawa na  watu wasiojulikana usiku wa  kuamkia Jumanne, Oktoba Mosi  2024 kwa kunyongwa na mkanda  wa suruali. 


Mwili wake ulikutwa umefunikwa  kitambaa chekundu usoni  

Taarifa za awali zinaashiria  mgogoro wa kugombea eneo la  uchimbaji madini ya ujenzi aina ya  moramu ni chanzo cha mauaji  hayo . 


Justine Masejo kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, amethibitisha tukio hilo akisema  uchunguzi umeanza kwa  kushirikiana na vyombo vingine  vya usalama,  

Masejo amesema bado chanzo cha  mauaji hayo hakijafahamika na  wameanza uchunguzi kujua kiini  cha tukio hilo kwa kushirikiana na  taasisi zingine za usalama mkoani  Arusha.


 Mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika Hospitali ya  Mount Meru.  

Jeshi la Polisi limesema linaendelea  na uchunguzi ikiwa ni pamoja na  ujumbe wa vitisho uliotumwa kwa  familia yake.  


"Uchunguzi zaidi unafanyika kwa  kushirikisha taasisi nyingine za  kiuchunguzi kutokana na ujumbe  wenye utata uliotumwa kwa ndugu  zake watatu Septemba 30, 2024  kabla ya kugundulika kwa mwili  wake katika Mlima Oldonyowas,'  


 Wakati huohuo, jirani na rafiki wa  karibu wa mke wa marehemu  Rehema John, amesema Mollel  alionekana mara ya mwisho  asubuhi ya Septemba 30, 2024  

Amesema alimuona saa tatu  asubuhi alipokwenda kunywa chai  nyumbani kwake na baadaye  aliondoka.  


"Jioni saa 12, rafiki yangu  aliniambia anakwenda polisi kutoa  taarifa maana anasikia mume wake  ametekwa na watu wasiofahamika  hivyo tukaenda kutoa taarifa na  kutakiwa kukaa saa 24 ndipo turudi  tena,' amesema  


"Baadaye saa mbili usiku shemeji  yake akampigia simu kumwambia  kuna watu wametuma ujumbe  kuwa wanaenda kumuua mume  wake kwa sababu amekataa kuachia  Mlima wa Moramu, amesema


  

Amesema familia ilianza msako na  asubuhi uligundulika mwili wake  katika msitu wa Mlima  Oldonyowas  

Mjomba wa marehemu  aliyejitambulisha kwa jina moja la  Mollel amesema alitumiwa ujumbe  kabla ya kupigiwa simu na watu hao  saa mbili kasoro.



"Wakati huo nikaamua kupiga hiyo  namba iliyotuma ujumbe akapokea  akasema wako watatu na  wamepewa pesa nyingi za  kuhakikisha wanamuua ndugu yetu  hivyo wanakwenda kumtundika juu  ya mti," amesema Mollel  

Steven Joram, jirani mwingine wa  Mollel amesema mauaji hayo yana  viashiria vya mgogoro wa eneo la  uchimbaji moramu ambalo alikuwa  akilimiliki.  


Ends....


Post a Comment

0 Comments