GACHAGUA NDO BASI TENA ATIMULIWA UMAKAMU WA RAIS KIBABE , APIGWA STOP KUGOMBEA NAFASI YOYOTE, SASA KURUDI MLIMANI !

By Ngilisho Tv-NAIROBI 

NAIROBI, Kenya – Bunge la Seneti nchini Kenya limepiga kura kumuondoa kazini Naibu Rais wa Taifa hilo, Rigathi Gachagua.


Wabunge wa seneti walipaswa kumtia hatiani katika shauri moja kati ya 11 yaliyokuwa yakimkabiri kiongozi huyo. Kwa sasa anakuwa Naibu Rais wa kwanza Afrika Mashariki kuondolewa ofisini kwa kura ya Maseneti.


Rais William Ruto anatajwa kuwa huenda akatangaza jina la mrithi wa Gachagua ndani ya saa 24 kuanzia sasa ambapo Wabunge watamuidhinisha katika kikao kilichopangwa kufanyika Ijumaa Oktoba 18.


Mapema Alhamis Bunge hilo lilipiga kura kuendelea na kesi ya kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua bila yeye kuwepo bungeni.


Maseneta walipiga kura ya kukiri kupinga hoja ya utaratibu wa kuahirisha vikao hadi Jumamosi, Oktoba 19, 2024.


“Kwa vile mchakato huu umefungwa na katiba, na ikizingatiwa kuwa muda unakamilika Jumamosi, dirisha pekee lililofunguliwa litakuwa kutangaza Jumamosi kama siku ya mwisho ya kusikilizwa kwa suala hili,” Amason Kingi alielekeza kabla ya maseneta hao kupiga kura.


“Ombi kama hilo linatumwa kwa Seneti, sio spika. Ninaelekeza karani kusambaza hoja ya kuahirisha.”


Kingi alikuwa ameomba Seneti kuahirisha kikao cha alasiri cha Alhamisi hadi Jumamosi, lakini maseneta hao walipiga kura kupinga pendekezo hilo.

Post a Comment

0 Comments