Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MAKAMU wa Rais,Dk,Philip Mpango anatarajia kufungua mkutano wa 53 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRICA) unaokutanisha Mabunge 19 ya Kitaifa katika Kanda ya Afrika utakaofunguliwa Oktoba 3 Jijini Arusha
Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha, Katibu Msaidizi wa CPA Kanda ya Afrika,Daniel Eliufoo alisema mkutano huo utaanza kesho(leo)Oktoba 1 hadi Oktoba 6 utafunguliwa rasmi Oktoba 3 mwaka huu kwaniaba ya Rais Samia Suluhu Hasani
Alisema tangu chama hicho kilipoanzishwa kimekuwa na mabadiliko makubwa ikiwemo ongezeko la idadi ya wanachama lakini pia kugawanywa katika Kanda tisa kati ya Kanda hizo Afrika ni mmojawapo ya Kanda ikiwemo Tanzania
Alisema miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni maspika 10 kutoka nchi mbalimbalimbali ikiwemo manaibu spika watatu hadi sasa washiriki 14 wamethibitisha ushiriki wa mkutano huo.
Alisema umoja huo wa Mabunge Kanda ya Afrika unaundwa na mabunge wanachama 65 kati ya hayo mabunge19 ni ya kitaifa na mabunge 46 ni mabunge ya majimbo .
"Tunaushiriki wa mabunge matano ya majimbo kutoka Afrika Kusini ikiwemo washikiri 280 katika mkutano huo weye lengo la kuhakisha mabunge hayo yanaleta amani,demokrasia ,utawala bora kwa nchi wanachama ikiwemo amani"
Akisisitiza lengo la mabunge hayo ni kuleta uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa asasi za umoja na huo ikiwemo dekokrasia,amani,utawala bora kwa nchi wanachama.
Ends..
0 Comments