Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI ,Mohamed Mchengerwa amemwagiz wakala wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA),kujenga kilometa sita kwa kiwango cha Lami katika barabara za ndani za jiji la Arusha .
Agizo hilo amelitoa jijini Arusha Oktoba 4 mwaka huu, wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kilombero baada ya kuhitinisha ziara yake ya kikazi jijini hapa, ambapo alipongeza viongozi wa mkoa huo kwa utekelezaji mzuri wa miradi mikubwa ya serikali.
Waziri Mchengerwa alimsimamisha jukwaani mtendaji Mkuu wa TARURA,Mhandisi Victor Seff aliyekuwa katika mkutano huo na kumwagiza kuhakikisha maelekezo yake ya kujenga kilometa sita ya barabara za kimkakati katika jiji la Arusha yanatekelezwa mara moja.
Aidha alilitaka jiji la Arusha kutumia fedha za ndani kiasi cha sh, bilioni 5 walizonazo kutekeleza ujenzi wa barabara za ndani ambazo zimechakaa.
"Nimeshatoa maelekezo katika maeneo ambayo jiji wanafedha nimewaambia anzeni mara moja kujenga barabara kwa kiwango cha lami kupitia fedha hizo walau kilometa 1.8 lakini pia jiji mmeniambia katika bajeti yenu mna fedha kiasi sh,bilioni 5 tumieni fedha hizo zitatosha takribani kilometa 6 kujenga barabara hizo kwa kiwango cha Lami"
Alisema maelekezo hayo yametokana na maombi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Paulo Makonda aliyetaka barabara zenye urefu wa kilometa 10 kujengwa kwa kiwango cha Lami katika jiji hilo.
Hata hivyo Mchengerwa alisisitiza ombi hilo aliliwasilisha kwa Rais Samia Suluhu ambaye aliagiza mtendaji mkuu wa TARURA kuwepo katika mkutano huo wa majumuisho ili kusikiliza maelekezo ya serikali .
"Maelekezo yangu kwa jiji la Arusha zipo barabara za kimkakati lazima zijengwe kwa kiwango cha Lami, nakuelekeza meneja wa Tarura mkoa wa Arusha nenda kafanye mapitio ili kujua barabara zipi zinafaa kuanza kujengwa"
Katika ziara yake jijini ARUSHA Mchengerwa alitembelea barabara ya Esso hadi Longdon yenye urefu wa kilometers 1.8 ambapo aliagiza ijengwe kwa kiwango cha Lami, hospitali ya wilaya aliyoagiza ujenzi wake uwe wa hadhi ya nyota tatu ama tano ili kuvutia watalii kupata matibabu , ujenzi wa uwanja wa Mpira pamoja na kutembele ujenzi katika Kituo cha Afya cha Levolosi na baadaye mkutano wa hadhara katika stand ya daladala Kilombero.
Ends.....
0 Comments