Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Chama Cha Mapinduzi ccm kimefanya uteuzi wa wagombea katika mitaa mbalimbali hapa nchini, ambapo kata ya Themi Mashariki jijini Arusha kimefanikiwa kuteuwa wagombea watakaokiwakilisha vema katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuwakabili wapinzani, unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 nwaka huu.
Mwenyekiti wa ccm katika kata hiyo Thomas Munisi alisema uchaguzi huo umeenda vizuri baada ya kuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama wa ccm ambao walifurika kutekeleza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi watakaochuana na vyama vya siasa.
Munis ambaye aliongoza mamia ya wanachama hao kupiga kura alisema wanaimani uteuzi walioufanya utaiwakilisha vema ccm katika mtaa huo katika uchaguzi wa serikali za mtaa unaoshirikisha vyama vingi na wanauhakika wataibuka na ushindi .
Aidha alisema chama cha mapinduzi kimekuwa kinara wa kulinda na kusimamia misingi ya demokrasia hapa nchini ndio maana kimekuwa na utaratibu wa kuchaguana kwa uwazi ili kupata viongozi wenye ushindani wanaouzika kwa wananchi.
Baadhi ya wanachama wa ccm, katika mtaa huo wa Themi Mashariki ,Wilson Kisuda alidai kwamba wanauhakika viongozi waliowachagua leo wataonesha upinzani mkubwa kwa vyama vya upinzani na watashinda na kuunda serikali ya mtaa huo.
Matokeo ya wagombea nafasi ya mwenyekiti aliyeshinda ni Godfrey Mushi kura 123,akifuatiwa na Edward Fundi kura 71 na Rahma kura 9
Ends...
0 Comments