AREMA YAPATA VIONGOZI WAPYA ,WENGI WATETEA NAFASI ZAO, RMO ARUSHA ATAKA UTATUZI WA MIGOGORO YA WACHIMBAJI

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


CHAMA cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Arusha (AREMA),kimefanya uchaguzi wake mkuu wa kikatiba na  kupata viongozi wake wapya watakaoongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Katika uchaguzi huo uliokuwa unasimamiwa na Afisa Madini Mfawidhi Mkoa wa Arusha RMO,Bertha Luzabiko, alimtangaza Alfred  Maswenya kuwa mwenyekiti wa chama hicho baada ya kupita bila kupingwa na kutetea nafasi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo. 


Wengine waliochaguliwa na kufanikiwa kutetea nafasi zao bila kupingwa  ni pamoja na Makamu Mwenyekiti, George Kessy ,Katibu Mkuu Isaya Letema na naibu Katibu Mkuu Vickta Mahango

RMO Luzabiko pia alimtangaza Prosper Tesha  kuwa mweka hazina Mkuu wa chama hicho akitetea nafasi yake, huku Josephine  akichaguliwa kuwa mweka hazina Msaidizi.


Viongozi wengine waliochagulika ngazi ya wilaya  ya Longido ni pamoja na Aquilino Mollel ambaye ni Mwenyekiti na makamu wake ni  Christopher Oloitimo .


Katika uchaguzi huo pia walichaguliwa wajumbe 6 wa kamati tendaji ambao ni Agnes Mushi,Joppa Malulu,Anjella Mawala,Samweli Msangi  Mathew Lomayan na Flavian Mamuya.


Nafasi za uwakilishi katika Shirikisho la vyama vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) TAIFA, ngazi ya mjumbe wa Mkoa ni Paschal Damian ,Elias Moshao(kundi la wafanyabiashara),Shedrack Mollel(Vijana),Milya Sambele(Wachimbaji wasio rasmi),Francis Mollel (Nidhamu na usuluhishi)Agnes Moshi(Afya na mazingira),Anjella Mawala (Ukaguzi wa Migodi),Joppa Malulu(mwakilishi wanawake) na George Nditika(habari siasa na Mahusiano).

Akiongea mara baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti wa AREMA, Alfred Maswenya alisema kuwa kazi iliyopo mbele yao ni kushughulikia migogoro  ya wachimbaji hususani mgogoro  uliopo eneo la machimbo  ya Ruby Mundalala wilayani Longido baina ya mwekezaji na watu wanaodai wapangishaji.


"Nashukuru  kupata nafasi hii kwa mara nyingine mimi na wenzangu tumejipanga kuhakikisha tunashughulikia migogoro yote ya wachimbaji kwa nafasi yetu"

Awali Afisa Madini Mkoa wa Arusha, Bertha Luzabiko aliwataka viongozi pamoja na wanachama wa AREMA kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza pato la serikali kupitia sekta hiyo.


Alisema sekta ya Madini kwa sasa inachangia pato la taifa kwa asilimia 9.2 na kuwataka wadau wa madini kuhakikisha sekta hiyo  inachangia kwa asilima 10 Ifikapo 2025.


Alisema changamoto za wachimbaji ni nyingi ikiwemo suala la mitaji na kuwataka wachimbaji kushirikiana na kuungana kwa pamoja kwani matarajio ya serikali ni kuona wachimbaji wanafanya shughuli zao kwa faida.


Aliwataka wachimbaji kuhakikisha wanakuwa na leseni za uchimbaji na kuzilipia kwani kwa kutofanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria na hatua za kuwafungia zitachukukiwa .

Mmoja ya wachimbaji wa madini ,Prosper Tesha ambaye pia ni Mhasibu wa chama hicho alisema katika sekta hiyo changamoto kubwa ni migogoro  sehemu za uchimbaji na kuwataka wadau wenye dhamana hiyo kushughulikia migogoro hiyo ili shughuli za uchimbaji zifanyike kwa ufanisi zaidi











Ends. 




Post a Comment

0 Comments