ALICHOKISEMA RAIS SAMIA KUHUSU MAJIKO YA GAMBO

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan
 amepongeza walimu 5000 wa shule za msingi na Sekondari Jijini Arusha kupatiwa mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake  kwa lengo la kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia .

Akizungumza kwa njia ya simu wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi na majiko hayo yaliyotolewa na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania kwa uratibu wa Mbunge wa Arusha Mrisho Gambo, Rais Samia alisema amepongeza hatua hiyo ya walimu  wa Arusha kupatiwa majiko ya gesi na kuahidi kuongeza majiko zaidi kwa walimu hao kwa siku za baadae.

“Nimepiga simu niwapongeze walimu kwa Mkutano mzuri ,Mbunge ameniambia leo mnamkutano wa nishati safi ya kupikia kwa hiyo niwapongeze kwa kuibeba hiyo ajenda.Niwaahidi tu mchango wangu katika hilo ndugu walimu  katika majiko yatakayotoka mimi nitakuja kujazia baadaye,”alisema Rais Samia na kusisitiza kuwa ajenda zao na changamoto za walimu anazifahamu na wanaendelea kuzifanyia kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omar Kipanga aliyekuwa mgeni katika maadhimisho ya walimu jijini Arusha kwa niaba ya Waziri wa Elimu  Profesa Adolf Mkenda alisema wanamshukuru Rais Samia kwa jitihada anazofanya za kuendelea kuhamasisha mapinduzi katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Tunamshukuru Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo pamoja na Oryx kwa kutoa mitungi ya gesi kwa walimu 5000 ili watumie nishati safi ya kupikia.Kama nilivyosema  kampeni Kya  Rais aliyotangaza Mei 8,2024 ni kwamba kila Mtanzania atumie nishati safi ya kupikia …

“Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia tumelibeba jambo hili na tumeanza na taasis zote za elimu ambazo  zinahudumiwa watu zaidi ya 100 kuanza kutumia nishati safi ya kupikia.Walimu 5000 wa Arusha ambao  wamepatiwa majiko ya gesi wanaandaliwa utaratibu wa kupatia elimu ya matumizi sahihi ya nishati  ili waweze kuishusha  kwa wananchi na wote tutumie nishati safi ya kupikia.


Awali Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania, Benoit Araman alisema kwa kushirikiana na Mbunge wa Arusha Mjini wameweza kuratibu walimu 5000 kupatiwa majiko hayo yenye thamani ya Sh.milioni 417.5 lakini dhamira yao ni kuona makundi mbalimbali yakiwemo ya walimu wanatumia nishati safi ya kupikia.


“Naomba  niwagusie Waalimu na Maprofesa sio tu kwa sababu tunawasherehekea leo siku ya Walimu bali naamini ninyi nyote ni kiungo muhimu kwa jamii na Taifa letu.Hivyo natoa ombi maalum kwa walimu kuwa mabalozi wa Nishati Safi ya kupikia.”

Akitaja baadhi ya faida ya kutumia nishati safi ya kupikia alisema nishati safi husaidia kuboresha afya kwani nchini Tanzania wananchi zaidi ya 33,000 wanafariki kila mwaka kutokana na kuvuta moshi na chembechembe zinazotokana na kuni na mkaa.Hivyo kupika kwa gesi ya kupikia oryx itaondoa changamoto hiyo.


Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo alisema wanatambua mchango wa walimu wote na katika kusherehekea siku ya walimu wameona kuna kıla sababu ya kuwapa zawadi ya jiko la gesi kwa kila mwalimu na wao wakawe mabalozi wa nishati safi.


“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amezindua mpango wa nishati ya kupikia na bado mpango huo ukaweka malengo mpaka kutoka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

“Kazi ya Rais ni kuonesha njia na sisi wasaidizi wake ni kumuunga mkono na leo tunakabidhi majiko ya gesi kwa walimu na hii ni kumuonesha mwalimu tunampenda na tunamtambua na sasa wakawe mabalozi wa nishati safi ya kupikia.Tunawashukuru Oryx kwa kumuunga mkono Rais Samia kwani gharama za majiko haya 5000 ni Sh.milioni 417.5 ,








Ends...

Post a Comment

0 Comments