WATAHINIWA 51,138 ARUSHA ,KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU DARASA LA SABA KESHO

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Jumla ya Watahiniwa wapatao  51,138 katika mkoa wa Arusha kesho Septemba 11,wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya darasa la saba katika vituo 801  mkoani hapa.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, afisa elimu mkoa wa Arusha,Abel Ntupwa alisema maandalizi yote yamekamilika na watahiniwa wote wanapaswa kuwa katika chumba cha mtihani saa moja kamili asubuhi. 

Alifafanua kuwa kati ya watahiniwa 51,138 wasichana wapo 26,201 na wavulana 24,937 na miongoni mwa watahiniwa hao 9095 watafanya mtihani kwa mfumo wa kiingereza.

"Kutakuwa na jumla ya vituo 801 na miongoni mwa vituo hivyo 20 ni vipya na wasimamizi wa mikondo watakuwa 2320 na watahiniwa wenye changamoti za kiafya ama ulemavu wowote watafanya mtihani kwa kupatiwa stahili zote"

Aidha alisema katika somo la hisabati kutakuwepo na mabadiliko ya ufanyaji wa mtihani, ambapo watahiniwa watalazimika kukokotea kwa vite do na kutoa jibu sahihi tofauti na miaka ya nyuma wanafunzi walikuwa wakisiliba kwa kuweka majibu pekee bila kuonyesha njia waliofanya kupata jawabu.

Aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wote wanaotahiniwa kufika kweny3 vituo mapema na kufanya mtihani.

Ends..



Post a Comment

0 Comments