Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)Mkoa wa Arusha ,imekutana na wafanyabiashara Mkoa wa Arusha kwa lengo la kutatua kero zao na kuwapatia elimu juu ya Mabadiliko ya kodi katika mwaka huu wa fedha 2024/25.
Akiongea na vyombo vya habari katika kikao kilichofanyika eneo la Majengo kati jijini Arusha,Meneja Msaidizi wa huduma kwa mlipa kodi Mkoa wa Kikodi Arusha, Peter Aliyona alisema kukutana na wafanyabiashara wa jiji la Arusha ni mwendelezo wa utaratibu waliojiwekea wa kujenga mahusiano ya karibu na wafanyabiashara na kutatua kero zao.
Alisema katika kikao hicho wafanyabiashara waliibua kero mbalimbali ikiwemo gharama za matengenezo ya mashine za EFDs pindi zinapoleta changamoto.
"Kikao hicho kimekuwa muhimu sana kwa kusikiliz kero za wafanyabiashara tumewaelimusha kuhusu mabadiliko ya kodi katika kipindi cha mwaka huu wa fedha na hii no kitii maelekezo ya kamishna wetu wa Mapato".
Aliwataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanatunza kumbukumbu zao pindi wanapotoa taarifa za changamoto ya mashine ili kupunguza kero zinazojitokeza.
"Hili ni zoezi endelevu tutakuwa tukikutana na wafanyabiashara kila la wiki siku ya Jumamosi ili kujenga urafiki na tunataka kila mfanyabiashara alipe kodi bila shuruti kwa kuona kwamba kodi ni wajibu wake kulipa"
Aliyona alisema wafanyabiashara wameomba kurejeshewa fedha pindi wanaponunua mashine za EFDs ila Meneja huyo alisema utaratibu huo huwa unafanyika kupitia makato ya kodi wanapolipa.
Naye Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara,Mkoa wa Arusha Kirenga Swai aliishukuru sana TRA kwa hatua waliojiwekea kwa kuanzisha utaratibu wa kuwafuata wafanyabiashara katika maeneo yao na kusikikiza kero zao na kuzitatua.
"Kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa ya kuwataka TRA kukusanya kodi halali imesaidia kuwaibya TRA kuanza kuweka mazingira mzuri ya kujenga mahusiano na wafanyabiashara na kusikiliza kero zao "
KATIBU wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani hapa,Ahmed Nuru Jamar ,aliiomba TRA kutumia utaratibu huu wa kukutana na wafanyabiashara nchi nzima hali itakayosaidia kujenga mahusiano na kuongeza mapato ya serikali.
Jamar aliwasihi watumishi wa mamlaka hiyo kuacha tabia ya kujifungia ofisini kusubiri kodi ya wafanyabiasha bali wajenge tabia ya kuwatembelea kwenye biashara zao na kusikiliza kero zao ikiwemo kuwapatia elimu.
"Leo TRA wametutembelea mbele ya maduka yetu kuja kusikiliza kero zetu ni jambo jema ila tunaomba TRA vikao kama hivi na wafanyabiashara kufanyika nchi nzima ,TRA wasikae maofisini wawafuate wafanyabiashara ambao ndio waajiri wao na kero zilizoibuliwa leo tunaomba zikatatuliwe"
Ends..
0 Comments