Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA,imewanoa wadau wa sekta ya habari pamoja na watangazaji kanda ya Kaskazini kwa kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia sheria na kanuni za leseni za utangazaji.
John Daffa Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji TCRA ,alisema semina hiyo imelenga kukumbushana wajibu na kuchukua maoni ya wadau wa habari lengo ni kuhakikisha tasinia ya habari inazingatia weledi ili kuliweka taifa katika hali ya Amani.
Alisema semina hizo ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara zimeleta tija kubwa katika tasini ya habari kwa wadau kujitathimini na kutoa taarifa zenye mizania na kuondoa ushabiki unaosababisha chuki na uvunjifu wa amani.
"Kupitia Semina hizi za kukumbushana wajibu kwa wadau wa habari na watangazaji tunaona Tija ipo na imesaidia kuimarisha weledi katika tasinia ya habari hasa utangazaji wenye kuzingatia mizania"
Daffa alisisitiza kwa kuwataka waandishi wa habari kuzingatia misingi ya uandishi wa habari ili kuepusha taifa kujiingiza kwenye machafuko ya kisiasa yasiyo na tija hasa kipindi hiki Taifa linapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani 2025.
Naye Meneja wa TCRA,kanda ya Kaskazini, Mhandisi Francis Mihayo alisema kikao cha wadau wa sekta ya habari katika Mikoa ya Manyara Arusha ,Kilimanjaro na Tanga kimelenga kuwakumbusha masuala ya sheria kanuni na maadili ya utangazaji.
Alisema Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, imebaini kuwepo kwa ukiukaji wa maadili ya utangazaji hususani katika maudhui yanayotangazwa na kurushwa mitandaoni.
Mhandisi Mihayo alisema kikao hicho pia kililenga kuwakumhusha kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani ili kuzijua kanuni za utangazaji zinazos8sitiza uwepo wa mizania .
"Kilichoanza kujitokeza ni kila mtu kurusha maudhui ambayo sio sahihi pamoja na mchanganyiko wa lugha kwa waliopewa leseni za utangazaji kwa kutumia Lugha zisizofaa wakati wa urushaji wa matangazo tifauti na wakati wakiomba leseni".
Aliwaomba kufuata masharti ya leseni zao katika utangazaji wa maudhui na kwamba mamlaka hiyo haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wanaokiuka mashari ya leseni zao.
Mmoja ya watoa Mada katika kikao hicho, Betty Mkwasa mjumbe wa kamati ya Maudhui TCRA, alisema kuwa kumekuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa waandishi wa habari tofauti na wakati wao wakifanya KAZI ya utangaza.
Mkwasa ambaye ni mwandishi mwandamizi wa habari aliyetumikia vyombo mbalimbali vikubwa hapa nchini alieleza namna tasinia hiyo ilivyovamiwa na waandishi wasio na taaluma na kuifanya ionekane haina maana tofauti na zama zao .
"Hivi sasa kumejitokeza watangazaji wasio na taaluma wamasema uongo ,hawafuati Mizania na kushabihikia matukio ,wakitumia vyombo vya habari kukashfu watu na kutweza utu wa mtu "
Aliwataka wadau wa habari kuilinda tasinia ya habari kwa gharama yoyote ili taaluma hiyo isiharibiwe kwa kuepusha upotoshaji wa habari.
Ends..
0 Comments