TAZAMA KISHINDO CHA MAPOKEZI YA KIONGOZI MKUU WA TWARIQA ATUA UWANJA WA NDEGE KIA KWA KISHINDO ,ATASHIRIKI AROBAINI YA KUMWOMBEA MARĂˆHEMU SHEIKH DARUWESHI MTI MKAVU

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

TAASISI ya dini ya Kiislamu ya Twariqa Qadiriya imepokea ugeni mzito wa Khalifa mkuu wa Taasisi hiyo kutoka  Zanzibar na Tanzania Bara Sheikh Jabir Al Ahdally ambaye ataongoza Dua ya Arobaini ya Kumwombea kiongozi wa Taasisi hiyo Sheikh Salimu Daruweshi Mti Mkavu aliyefariki Agosti 21,2024



Akiongea na vyombo vya habari Leo septemba 29,2024 Msemaji wa idara ya habari wa taaisis ya Twariqa, Sheikh Haruna Husein alisema ujio wa kiongozi huyo ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaotarajiwa kufika jijini Arusha kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo dua ya marehemu Daruweshi.


"Leo tumempokea Khalifa wetu Mkuu kutoka Zanzibar ambaye ni miongoni mwa masheikh wetu wakuu ambaye tutakuwa naye katika sherehe yetu kuu ambayo inaanza leo na kesho kwa ajili ya dua ya kiongozi wetu marehemu Sheikh Salimu  Daruweshi"


Naye Sheikh Jabir Ahdally Khalifa Mkuu wa Zanzibar na Tanzania Bara aalipongeza mapokezi ya viongozi wa Twariqa Mkoa wa Arusha akitokea uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) na kusema kuwa ujio wake umelenga kushiriki dua ya Arobaini ya Marehemu Sheikh Salimu Daruweshi .


"Nimekuja kurishiki Arobaini ya marehemu Sheikh Salimu Daruweshi itakayofanyika kesho Septemba 30,2024 na wiki itakuwa nzito sana kutokana na mlolongo wa shughuli mbalimbali"


Akiongelea Maadhimisho ya Arobaini ya Sheikh Salimu Daruweshi, Khalifa  mkuu wa Taasisi ya Twarika Mkoa wa Arusha,shaikh Mohamed Omari alisema maandalizi ya Sherehe hiyo yamekamikika.


Alisema Arobaini ya marèhemu  Daruweshi itafanyika makao kesho makuu ya Twariqa  ikitanguliwa na dua ya kumrehemu na baadaye waumini wa dini hiyo watakesha makaonmakuunya Twariqa. 








Ends...

Post a Comment

0 Comments