TAKUKURU ARUSHA YANOA MAKUCHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA,YATAJA MAENEO MATANO HATARI AMBAYO RUSHWA INAPENYESHWA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, imebaini maeneo matano yenye ushawishi wa rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2025.

Akizungumza leo katika halfa ya utoaji elimu dhidi ya mapambano ya rushwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mkoani Arusha, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo alisema maeneo hayo ni uteuzi wa wagombea ngazi ya chama, kampeni,upigaji kura, kujumlisha na kutangaza matokeo pamoja na kushughulikia malalamiko.


Alisema katika mchakato wa wagombea ndani ya chama kumekuwa na rushwa ikiwemo kampeni pia wagombea baadhi wanatoa hela ikiwemo rushwa ya vyakula , kanga, ahadi za ajira kwa wapigakura ikiwemo kutumia lugha za vitisho nguvu au mabavu ili kuwalazimisha kupiga kura au kuwazuia wasipigekura.


“Wananchi msikubali kupata kiongozi anayetaka madaraka kwa kutoa fedha maana hatakuwa kiongozi bora wa kuleta maendeleo lakini pia wanaotoa fedha kununua uongozi wajue sheria zipo na Takukuru ipo macho inafuatilia kila kitu ikiwemo kuchukua hatua stahiki,” alisema.


Alizitaja athari za rushwa katika chaguzi za kisiasa ni pamoja na kumnyima mpigakura haki ya kumchagua mgombea amtakaye, ikiwemo kumnyima haki mgombea asitetoa rushwa kuwa kiongozi ikiwemo kiongozi aliyechaguliwa kutumia muda wa uongozi wake kurejesha fedha zake na si kuleta maendeleo kwa wananchi sanjari na kukwamisha utoaji wa haki.

Akijibu Ubutu wa Takukuru wakati wa mchakato wa uteuzi wa wagombea ambako ndiko rushwa inatembea, Ngailo  alisema suala la rushwa sio la taasisi pekee ,bali kila mtu anapaswa kuichukia rushwa na kutoa ushirikiano kwa Takukuru ili kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wahusika

Ends...

Post a Comment

0 Comments