SHANGILIENI MARATHON KUTIMUA VUMBI ARUSHA,MEYA KUMENYENA NA DED ARUSHA DC ,ATAKA WATU WAJITOKEZE KUBORESHA AFYA ZAO

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Meya wa jiji la Arusha Maxmilian Iranghe amewataka wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake, kujitokea kushiriki mbio za SHANGILIENI Marathon ambazo zimekuwa zikiandaliwa mahususi kwa ajili ya kuimarisha Afya na kusaidia jamii iliyopo pembezoni kwa kuchangia huduma ya afya .


Akiongea na waandishi wa  habari wakati wa hafla ya kutambulisha mbio hizo zinazojulikana kwa jina la SHANGILIENI MARATHON ikiwa ni msimu wa pili kuandaliwa na kanisa la Anglikana, alisema jamii inawajibu wa kushiriki mbio hizo kama sehemu ya kujikinga na maradhi nyemelezi, zinazotarajiwa kufanyika September 14,mwaka huu na 


Mratibu wa SHANGILIENI MARATHON, Scolastica Porokwa alisema msimu wa pili wa Mbio hizo watu zaidi ya 1000 wanatazamiwa kushiriki na wamelenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii ambazo hazifikiwi kirahisi Kwa kupeleka huduma za Afya yakiwemo madawa vyakula na mavazi hasa jamii ya  Wahadzabe iliyopo wilayani Karatu.


"Kiingilio katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika September 14,ni shilingi 35,000 na katika fedha hizo utapewa tisheti na medali pamoja na zawadi mbalimbali na fedha hizo zitakwenda Kusaidia jamii  ya pembezoni hususani wahadzabe"


Alisema kuwa mashindano hayo ya shangilieni Marathon katika msimu uliopita mwaka jana 2023 yalikuwa na mafanikio makubwa baada ya kuwafikia jamii ya pembezoni zaidi ya 800  na akina mama 400 walipatiwa huduma bure za kiafya.


"Mbio zetu zitakuwa kati ya kilometa 5 hadi 21 na washiriki watapata huduma zote stahili"Alisema Porokwa.



Ends...














Post a Comment

0 Comments