SERIKALI YATANGAZA VIJIJI 12,333 KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI YA MITAA,VIMO 65 VILIVYOFUTWA NGORONGORO, MWENYEKITI NGORONGORO AIPONGEZA SERIKALI ASEMA WANANCHI WAMEHAMASIKA!

  Na Joseph Ngilisho ARUSHA


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI,  Mohamed Mchengerwa ametangaza kuwa jumla ya Vijiji 12, 333, mitaa 4,269 na Vitongoji 64, 274 vitashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.


Akiongea Jijini Arusha leo Jumatatu Septemba 16, 2024 kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mchengerwa amewaambia wanahabari kuwa kwenye orodha hiyo kumejumuishwa maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa tangazo la serikali ambayo pia yalihusisha Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha.


"Matangazo haya yanajumuisha maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa Tangazo la serikali namba 673 na 674 ambayo yalihusisha pia Tarafa ya Ngorongoro. Lengo la hatua hii ni kuhakilisha kuwa maeneo haya yanapata uwakilishi mzuri kiutawala pamoja na huduma za kijamii na kiuchumi zinazowiana na mahitaji ya wananchi." Amesema  Waziri.


Akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Paul Christian Makonda, Mchengerwa amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo katika kuunda serikali ya wananchi kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la mpigakura kwa mustakabali wa maendeleo na kuendeleza juhudi za serikali katika kujitafutia maendeleo endelevu.


Alisema lengo la hatua hii ni kuhakilisha kuwa maeneo haya yanapata uwakilishi mzuri kiutawala pamoja na huduma za kijamii na kiuchumi zinazowiana na mahitaji ya wananchi.


Mchengerwa pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo katika kuunda serikali ya wananchi kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la mpigakura kwa mustakabali wa maendeleo na kuendeleza juhudi za serikali katika kujitafutia maendeleo endelevu.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mohamed Bayo alisema wamepokea kwa furaha tamko la waziri kuunganisha vijiji 65  pamoja na vitongoji 242 vilivyokuwa vimefutwa wilaya ya Ngorongoro. 


"Tumepokea kwa furaha sana tamko la Serikali kurejesha vijiji 65 na vitongoji 242 vilivyokuwa vimefutwa kurejeshwa na  kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa"

Bayo alisema kuwa  tayari uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukihamasisha wananchi kushiriki uchaguzi huo na idadi kubwa ya wananchi wamehamasika.


Awali Hali ya Ngorongoro ilikuwa tete, hivyo kupelekea kufanyika maandamano ya yaliyowahusisha wenyeji wa eneo hilo ambao ni jamii ya kifugaji ya Wamaasai yaliyofanyika mnamo Agosti 18, 2024. 

Maandamano hayo, yaliyoshirikisha wanaume, wanawake, na vijana wa kabila la Wamasai, yalipinga kunyimwa huduma za msingi, ubaguzi, na haki yao ya kuishi katika ardhi ya Ngorongoro. 


Waandamanaji walibeba mabango na walifunga barabara yenye shughuli nyingi ya Ngorongoro-Serengeti.


Maandamano haya yalijiri wakati ambapo serikali inatekeleza mpango wa kuwahamisha Wamasai zaidi ya 110,000 kutoka Ngorongoro kwenda maeneo mengine kama Msomera, Sauni, na Kitwai, umbali wa zaidi ya kilomita 300 kutoka makazi yao ya sasa. 


Serikali inaeleza kuwa uhamisho huu ni muhimu kwa ajili ya kuhifadhi Eneo la Hifadhi la Ngorongoro, ambalo ni sehemu ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.


Rais Samia Aihakikishia Ngorongoro Uchaguzi Kuendelea Kama Ulivyopangwa


Ingawa serikali inasisitiza kuwa uhamisho ni hiari, Waziri wa Maliasili na Utalii na msemaji wa serikali walieleza kuwa serikali ina mpango wa kuja na sheria itakayoondoa hali ya sasa inayoruhusu makazi ya watu ndani ya Ngorongoro.


 Ili kuvutia wakazi kuhama kwa hiari, serikali imeendelea kujenga nyumba bure kwa wahamiaji na kutoa usafiri wa kutoka Ngorongoro hadi Msomera. 


Hadi Aprili 2024, serikali iliripoti kutumia Shilingi bilioni 286 katika juhudi za uhamisho huo, ambapo takriban wakazi 8,364 wamehamishwa tangu Julai 2022.


Miongoni mwa madai ya Wamasai wengi waliobaki Ngorongoro wanailalamikia serikali kwa vitendo vya kibaguzi, ikiwemo mahitaji ya vibali maalum vya kuingia na kutoka Ngorongoro. 


Naye katibu Tawala mkoa wa Arusha Musa Miseile aliwataka viongozi wa mkoa wa Arusha kuhalikisha wanaenda kusimamia vema uchaguzi huo bila kuonesha upendeleo wowote wa vyama vya siasa kuhakikishabuchaguzi unakuwa huru na wahaki.









Ends...


Post a Comment

0 Comments