PROF MUSHI ATAKA AFRIKA IFIKIRIE KUZALISHA UMEME WA UHAKIKA KUTUMIA NISHATI YA NYUKLIA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

 

NAIBU katibu Mkuu wa Sayansi na Teknolojia Prof.Daniel Mushi amezitaka nchi za ukanda wa  Mashariki Afrika EAPP, kufikiria namna ya kuanza kutumia nishati mbadala ya umeme unaotokana na madini ya Nyuklia kuzalisha  umeme wa uhakika ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.


Frof Mushi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa mafunzo kwa wataalamu wa nishati ya umeme kutoka makampuni makubwa ya umeme nchi 13 za ukanda wa Mashariki Afrika (EAPP).


Alisema nchi nyingi za Afrika  zina uhaba wa umeme hivyo aliwataka wataalamu hao waanze kufikiria vyanzo vipya vya kupata umeme wa uhakika ikiwemo matumizi ya madini ya Nyuklia.


"Tunahitaji kufikiria vyanzo mbadala vya kupata umeme wa uhakika ,niwakati wa nchi za Afrika kuzaliza umeme kwa kutumia chanzo cha umeme kupitia madini ya nyuklia ili tupate umeme wa kutosha kwani viwanda vyetu vingi vinavyojengwa kwa sasa vinahitaji umeme wa uhakika"



Alisema Tanzania kuna madini mengi ya uranium ambayo yanaweza kutumika kuzalisha umeme na nchi kuwa na umeme wa kutosha na kuweza kuuziana na nchi nyingine ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa.


"Tunataka kutumia ujuzi wa chi ambazo zimefabikiwa kutumia nishati ya umeme wa madini ya nyuklia "


Msimamizi wa mafunzo  Kanda ya Afrika , dkt Dennis Mwalongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, alisema mkutano huo unalenga kuwaongezea ujuzi 

wataalam hao kutoka nchi  wanachama wa Easterm Africa Power Pool (EAPP) ambao watajadili kwa wiki mbili namna ya upatikanaji wa nishati ya umeme kupitia vyanzo mbalimbali vya asili ikiwemo joto  Ardhi na matumizi ya madini ya nyukilia.


"Wataalamu hawa wamekutana kwa ajili ya kujadili mahitaji ya umeme kwa kanda ya Mashariki katika kipindi cha miaka 50 ijayo ukizingatia kwamba matumizi ya umeme katika kanda ya Afrika Mashariki yamekuwa makubwa kwa sababu watu wanaongezeka"


Mwalongo alisema mafunzo hayo ya wataalamu wa nishati ya umeme,yameandaliwa na shirika la Kimataifa la nishati za Atomic pamoja na EAPP na watajadili pia makadirio ya mahitaji ya umeme katika kipindi cha  miaka 50 ijayo kwa kutumia data za kidemographics (idadi ya watu) .

"Mfano kutoka kwenye gesi , maji , just, na katika maeneo mengine yanayozalisha Nishati lengo letu ni kuhakikisha tunagawana nsishati hii kwani nchi moja ikiwa na Nishati nyingi unaweza kumgawia mwingine ambapo mango huo umefanikiwa Kati ya Tanzania na Kenya, Nchi ya Kenya na Ethiopia" Alisema Mwalongo.

 

Alizitaja  nchi za Ethiopia na Kenya  ambazo zimepiga hatua kubwa katika vyanzo vikubwa vya nishati ya umeme na kuweza kuuza umeme kwa nchi nyingine jambo ambalo wataalamu hao watajadili na kuibuka na majibu ya jinsi gani nchi zingine wanachama zinaweza kuwa na vyanzo vya nishati.


Naye Katibu mkuu  wa shirika la EAPP,James Wahogo alisema nchi wanachama wa EAPP zinauzalishaji Mkubwa wa umeme na wataangalia namna ya nchi hizo ziweze kupeana umeme kwa kuuziana.


"Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka vyanzo asili ikiwemo Gesi na tunaimani katika kipindi cha mbeleni itakuwa na umeme mwingi wa ziada na kuziuzia nchi za jirani"


Wahogo alizitaja nchi hizo zinazounda umoja wa EAPP kuwa ni Burundi,Comoro, DRC Congo,Djibouti, Misri,Eritrea,Ethiopia, Kenya,Libya, Madagascar, Malawi,Rwanda,Shelisheli,Sudan Kusini ,Sudan,Tanzania, Uganda na Zambia.


Mmoja ya washiriki kutoka Tanesco idara ya Mipango, Mhandisi Mwandamizi Alex Heruka alisema mafunzo hayo ya kitaalamu yanalenga kufanya makadirio ya matumizi ya umeme kupitia vyanzo mbalimbali vya nishati. 


"Ushiriki wetu katika mafunzo haya utasaidia kujifunza  makadirio kupitia vyanzo mbalimbali vya kufua umeme kama Maji,Gesi ,Makaa ya Mawe ,Jua ,Upepo Nk na hii itasidia kuepuka athari za mabadiliko ya tabia ya nchi"


Alisema kwa sasa Tanzania imekamilisha kuunganisha mifumo ya umeme kwa  kujenga  laini za umeme kutoka  Tanzania kwenda Zambia na ipo katika hatua ya upembuzi akinifu katika nchi za Zambia , Uganda , DRC Congo ,Malawi ,Rwanda na Burundi ili pale panapotokea nchi hizo zinaupungufu wa umeme waweze kuziuzia.










Ends..











Post a Comment

0 Comments