Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema serikali haitakuwa kikwazo kwa shughuli zinazoendeshwa na asasi za kiraia (AZAKI) na kuwataka kuwa na jukumu la kutafuta fursa zaidi katika kujipatia maendeleo.
Akizindua maadhimisho ya AZAKI yaliyokutanisha washiriki zaidi ya 600 yanayofanyika jijini Arusha ,Prof Mkumbo alisema lengo la Dira ya Taifa kwa miaka 25 ijayo ni kuondoa umaskini na kuweka ustawi kwa wananchi wote kwa serikali kuanza kuwekeza katika elimu zaidi.
Prof .Mkumbo alisema kuwa,serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa asasi hizo na kamwe haitakuwa kikwazo kwa shughuli za Asasi za kiraia zinazoendelea hapa nchini .
Amesema asasi za kiraia zina jukumu la kutafuta fursa kwa serikali ,sekta binafsi pamoja na Asasi, hivyo serikali itakuwa pamoja nao na kuwaunga mkoani .
Naye Rais wa Shirika la Foundation for Civil Society FCS Dkt. Stigmata Tenga alisema asasi ni daraja kati ya sauti za mwananchi ,dira za wananchi na thamani ya mwananchi hivyo kwa muda wa wiki moja watakaa pamoja wataongelea namna watakavyofanya kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Aliongeza kuwa rasili Mali watu ndo nguvu kazi na ndio inayoweza kuleta mabadiliko na kuhakikisha mwananchi wa Tanzania ameweza kuendesha maendeleo yake mwenyewe bila kusaidiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Foundation for Civil Society ,Justice Rutenge alisema kuwa , wanahitaji kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa vikwazo vilivyopo na kushughulikia changamoto za kimuundo na kimfumo na kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
“Tunataka kuvuka vikwazo vikubwa kwa kufanya kazi pamoja ili kuondoa vikwazo kama afya, kilimo, biashara na utawala bora kwani Sisi kama wadau tuna maoni mengi sana ya kuweza kuchangia ili kuendana na kasi ya dira ya maendeleo. “
Washiriki katika Wiki ya AZAKI Mkurugenzi wa Taasisi ya Usawa wa Ukuaji iliyopo Dar es salaam,Jane Magigita alisema wanataka kubadilisha mfumo wa mawazo hasi unaobadilisha maono kuwa ya kikoloni hali inayotishia watu wengi na kudumaza maendeleo yao.
Alisema kuna umuhimu wa kushirikiana na makampuni makubwa na viwanda vikubwa ili kwa pamoja kuweza kubadilisha maisha ya wananchi.
“Msisitizo wa Tanzania tuitakayo na lengo la serikali ni kila Mtanzania kuishi maisha mazuri yenye ustawi huku tukichagiza jitihada za serikali katika kuleta maendeleo na mabadilko kwa watu wa makundi maalum” alieleza Magigita.
Wiki ya AZAKi 2024 inapoendelea, ujumbe wa ushirikiano kati ya AZAKi, serikali, na washirika wa kimataifa ni muhimu katika kutatua changamoto za nchi na kuhakikisha kuwa kuna ushirikishwaji zaidi na zaidi. siku zijazo endelevu.
"Kwa kuunganisha nguvu, tutaweza kutengeneza mustakabali wa Tanzania kuwa bora," Mignucci alihitimisha, akirejea dhamira ya pamoja ya washirika wote wa maendeleo.
Mundle alisisitiza kujitolea kwa Kanada: "Tumejitolea kufanya kazi pamoja na AZAKi, serikali, na wabia wengine ili kutimiza maono ya jamii yenye haki na ustawi ambayo inanufaisha Watanzania wote."
Kwa kuendelea kuungwa mkono na wabia hawa, asasi za kiraia za Tanzania zinaendelea kuwa mstari wa mbele katika kukuza utawala bora, kuendesha maendeleo ya mtaji wa watu, na kuhakikisha uwajibikaji unaohitajika ili kuthibitisha taifa kwa siku zijazo.
Ends.
0 Comments