Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MFANYABIASHARA Maarufu katika jiji la Arusha(Jina linahifadhiwa),ameomba msaada wa Kisheria baada ya mke wake wa ndoa aliyemtaja kwa jina moja la PRISCAR kumfilisi kwa kumwibia fedha katika biashara yao ya Supermarket iliyopo Sanawari Arusha na kujenga nyumba tatu za kisasa, kununua magari manne na bajaj 3 kwa siri bila mume kujua.
Aidha mfanyabiashara huyo ambaye ameamua kuyakimbia makazi yake kukwepa kero na maudhi ya mkewe, amewaomba wataalamu wa masuala ya Kisaikolojia kumsaidia kumjenga kiakili kutokana na mawazo mabaya yanayomzonga kichwani mwake akihisi anaweza kufanya kitu kibaya maishani.
Akiongea kwa uchungu baada ya kuwaonesha wandishi wa habari nyumba hizo zilizojengwa na mkewe katika eneo la Uswahilini Kisiwani na Muriet,alisema tangu mkewe ameanza kumwibia kidogo kidogo ni zaidi ya sh,milioni 250 zimepotea katika biashara yake.
Alisema kwa namna alivyompenda mke wake na kumwamini katika kipindi cha miaka 30 ya ndoa yao, hakuamini kama angeweza kumfanyia unyama wa aina hiyo na kumwacha mweupe pee!
"Mimi ni mfanyabiashara wa zaidi ya miaka 30 hapa Arusha,mwaka 1996 nilibahatika kuishi na mke wangu na baada ya miaka nane nilifunga naye ndoa kanisani "
"Baada ya kuanza kuishi naye nilimwamini kwa asilimia 99 kwa sababu katika maisha yangu najiamini mimi mwenyewe na mke wangu,simwamini mtoto wala ndugu yangu yoyote"
"Nilimkabidhi mke wangu biashara zote asimamie mauzo lakini chaajabu baada ya muda alibadilika na kuanza kiburi akawa mlevi sana"
"Mwaka 2016 nilipata kiharusi(Stroke)nikamuuliza hii Stroke nimepataje akanijibu na bado.. nililazwa hospitali ya Seliani wiki mbili na baadaye nilihamishiwa nchini India"
"Niliporejea nchini nilipata taarifa kupitia kuwa mke wangu anajenga nyumba nyumba kwakweli sikuamini, siku moja alikuja ndugu yake na kuniambia kuwa mama yake na mke wangu(Mama mkwe) anasimamia nyumba ya Mke wangu.
Niliamua kufuatilia siku moja mke wa ndugu yake alinipigia simu na kuniambia kuwa mume wake pamoja na mke wangu(Priscar)kuna vitu wanavifanya,kuna nyumba anasimamia,
Siku moja niliamua kufuatilia na kukuta amejenga nyumba moja ya kisasa eneo la Uswahilini Kisiwani ina vyumba vinne na nyingine nikagundua ipo eneo la Muriet karibu na nyumba ya Mbunge Mrisho Gambo ina wapangaji na wanakula kodi yeye na mama yake.
"Nilirejea nyumbani na kumwambia mke wangu kuwa nimegundua hizo nyumba ulizojenga ninachotaka ni kuziuza ili tuendeleze biashara ,alikubali lakini alisema ngoja akamweleze mama yake ,aliporejea alikuwa amebadilika na kuniambia kuwa kama nazitaka nizinunue ama niende mahakamani"
"Wakati hayo yanaendelea mke wangu alikuwa bado dukani akiendelea na biashara yetu ya Supermarket ,siku moja nilimfuma kwa macho yangu akiweka fedha kwenye maziwa sh,80000 nilimuuliza kwanini anachukua fedha zote hizo hakunijibu ,siku nyingine nilikuja ghafla dukani nikakuta anaficha kwenye pochi sh, 50,000 nilipomwambia arudishe alisema sio lazima kurudisha basi niliamua kupotezea na kumwacha kuepusha ugomvi"
Alisema wakati hayo yanaendelea duka iliendelea kufilisika na kushindwa hata kurejesha mikopo kulipa, kodi za serikali
Pia aligundua mkewe amejenga nyumba nyingine moja wilayani Karatu ,amenunua gari nne aina ya Noar na Bajaj tatu mali zote hizo alimwandikisha ndugu yake mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Nyangusi.
Alisema aliamua kupeleka malalamiko hayo kanisani na mkewe alipohojiwa alikiri na kukubali kwa maandishi kurejesha mali hizo lakini mama mkwe wake aliamua kuficha nyaraka na kuzibadilisha umiliki wa mali hizo.
Alisema kuwa matukio yote hayo yamefanyika ndani ya miaka 25 ya ndoa yao huku umiliki wa nyumba hizo akiwamilikisha ndugu zake aliowataja kwa jina la Mathayo na nyangusi na kwamba amegundua mkewe anajenga nyumba nyingine Mkoani Mwanza .
Alisema baada ya kugundua hayo mkewe alianza kudai waachane kisheria mahakamani ili wagawane mali jambo ambalo Mume anaomba ushauri wa kisheria.
Mfanyabiashara huyo ambaye kwa sasa ameyakimbia makazi yake na kwenda kusikojulikana , alisema anahisi mkewe amemfanyia ushirikiana kwani amekosa nguvu ya kumfukuza ama kumwondoa dukani hivyo anaomba msaada kwani anahisi kuchanganyikiwa.
"Niliamua kuchukua nguo zangu na kuondoka nyumbani na kuacha kila kitu sina amani hata watoto amewarubuni wanidharau hawaniheshimu kila kitu nafanyiwa na msichana wa kazi na mke wangu amekuwa mtu wa kunywa pombe na kunitukana "
Akiongea kwa njia ya simu Priscar ambaye yupo Safarini Musoma ,alisema kuwa matatizo ya kifamilia baina yake na Mumewe yemeshakuwa sehemu ya maisha yao na hakuna jipya kati yao.
Alishindwa kukataa ama kukubali kama amekuwa akimwibia mumewe katika kipindi cha miaka 25 na kujenga nyumba kadhaa,kununua magari na Bajaji kwa siri ila alisema kuwa kama ana uhakika na suala hilo aende mahakamani.
"Kwanini aendelee kulalamika hadi kwenu si aende mahakamani msaidieni aende mahakamani "Alisema kwa kujiamini
Hata hivyo alisema bado anampenda mume wake na hajawahi kumnyima hata unyumba ila hata acha kusikiliza ushauri wa mama yake mzazi.
"Mwambie aende ofisi ya serikali ya mtaa katika eneo husika na akahoji mikataba ya ununuzi wa viwanja na mmiliki halali wa nyumba hizo"
"Huwezi kukaa na mwizi humwambii chochote huendi mahakamani bado unaendelea kukaa naye hushangai hata wewe Mwandishi??alihoji Priscar
Priscar alienda mbali kwa kumtuhumu muwewe kutokuwa mwaminifu katika mahusiano yao ya ndoa akidai mumewe anamahawara wengi wanaweza kujaa Costa mbili jambo ambalo mume alikanusha na kudai sio kweli ila analenga kubadilisha hoja ya msingi.
Ends....
0 Comments