KLABU YA MAZOEZI YA POLISI JAMII USIPIME UKIMALIZA MBIO UNAGONGA SUPU NZITO,CRDB YATIA MGUU YATAKA MAZOEZI YATUMIKE KUIMARISHA AFYA NA MAHUSIANO .

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Klabu ya Mazoezi  ya Arusha  Polisi Jamii Jogging  inayoundwa na Askari polisi wa jiji la Arusha ,raia na taasisi mbalimbali kwa kushirikiana na Benki ya CRDB Mkoani hapa,leo imefungua ukurasa mpya wa mazoezi yatakayokuwa yakifanyika kila wiki siku ya jumamosi.






Akiongea na waandishi habari Mratibu wa Mazoezi hayo yenye lengo la kuimarisha afya na ukakamavu wa mwili ,DITRICK MTUKA alisema Klabu hiyo kwa sasa ni rasmi baada ya kupata mdhamini wa uhakika  benki ya CRDB na wiki ijayo watachagua Uongozi wa klabu hiyo.


MTUKA ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Sekei,alisema awali klabu hiyo ilikuwa ikifanya mazoezi na baadaye kutawanyika ila kwa sasa wanaishukuru  benki hiyo kwa kudhamini klabu hiyo  kwa kuwapatia maji na supu baada ya kumaliza mazoezi ya kukimbia na viungo.
"Tunawashukuru wenzetu wa Benk ya CRDB kwa kudhamini klabu yetu ya mazoezi naimani kwa sasa tutapata maji na Supu baada ya mazoezi, hii itahamasisha hata wasio shiriki kujiunga nasi"Alisema MTUKA.

Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Kaskazini, Cosmas Sadat alilishukuru jeshi la polisi kwa kubuni na kuanzisha klabu ya mazoezi ambayo itasaidia kuunganisha jamii ya watu wa Arusha. 

Alisema benki ya CRDB imeamua kushiriki katika  Jogging Klabu ili  kujenga mahusiano ya kiafya , kibiashara na kubadilishana mawazo.

Alisema klabu hiyo itasaidia kuunganisha vijana wa Arusha  kuwa na mahusiano mazuri na jeshi la polisi na kuwez kuzalisha uchumi wa taifa na kupunguza matukio ya uhalifu yasio ya lazima.

"Kupitia Arusha polisi jamii Jogging Klabu itasaidia kujenga Afya na kuimarisha miili yetu pia  jeshi la polisi litajenga mahusiano mazuri na raia na kuendelea kudumisha amani"






Ends. 


.


Post a Comment

0 Comments