KISHINDO CHA DCP NG'ANZI ARUSHA CHASHTUA ,AWANASA MADEREVA WAZEMBE NA WALEVI ,FAINI YAKE USIPIME AKUSANYA MILIONI 9 KWA SAA CHACHE, AMPONGEZA WP ALIYEENDESHA BASI

Na. Joseph Ngilisho ARUSHA


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini , DCP Ramadhan Ng’anzi ameendesha operesheni  kabambe ya kushtukiza katika mkoa wa Arusha na kufanikiwa kuwanasa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani ikiwemo ulevi na kuwatoza faini ya sh,milioni 9 kwa siku moja.

Akiongea na vyombo vya habari katika eneo la ukaguzi la Ngaramtoni ya Chini,jijini hapa,alisema Ukaguzi wa vyombo vya moto ni zoezi endelevu na limelenga  kudhibiti ajali za barabarani kwa kufanya kaguzi za kushtukiza na alifanikiwa kukagua magari zaidi ya 300 na kutoza faini.


DCP Ng’anzi amebainisha kwamba katika kikao kilicho fanyika hivi karibuni katika Shule ya Polisi Tanzania iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Rais  Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi,alilitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linadhibiti ajali hapa Nchini zinazopoteza maisha ya watu wengi.

DCP Ng’anzi alisema kuwa  operesheni hiyo ni endelevu na inafanyika nchi nzima huku akiwaomba abiria kutoshabikia mwendokasi wa mabasi na badala yake watoe taarifa kwa Jeshi hilo ili madereva wazembe wachukuliwe hatua za kisheria.

"Lengo la operesheni hii ni kuona kwamba ajali nyingi ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu na wengine kupata majeraha zinadhibitiwa ipasavyo"


Aliongeza kuwa "Rais Samia katika kikao cha maafisa wa polisi katika shule ya polisi mjini moshi,alitupa shime na kututaka tuongeze  juhudi za  kupambana na ajali za barabarani na kufuatia maagizo hayo masaa machache tulitawanyika nchi nzima kuendesha operesheni ya nguvu"

Alisema katika operesheni hiyo wamebaini kuwepo kwa madereva wanaotumia kilevi pamoja na kutafuna mirungi iliyopigwa marufuku hapa nchini,kuharibu mfumo wa kidhibiti mwendo,kujaza abiria kupita kiasi ,mwendo kasi na makosa hayo kuwa sehemu ya chanzo cha kusababisha ajali.

Alisema pia wamekuwa wakitoa elimu kwa abiria wa mabasi kutoshabihikia mwendo kasi wa mabasi na kuwataka kutoa taarifa kwa askari wa usalama barabarani kwa dereva anayeendesha gari kwa mwendo kasi.

Alisema operesheni ya ukaguzi wa magari inafanyika kwa saa 24 kwani mchana wanafanya ukaguzi wa gari zote ila usiku wanafanya ukaguzi wa magari makubwa ya mizigo na mabasi ya usiku na kuchukua hatua kwa madereva wanaokiuka sheria.

"Serikali yetu baada ya kuruhusu mabasi kutembea kwa saa 24 tutafanya ukaguzi usiku kuona kwamba wanazingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ,mwaka huu tunakauli yetu endesha salama ufike salama"

Katika hatua nyingine DCP Ng'anzi kwa niaba ya mkuu wa polisi nchini IGP, Camilius Wambura alimpongeza askari Polisi wa Kike  WP Koplo Sheila Mwengo  kwa kuliletea sifa nzuri Jeshi la Polisi wakati akitekeleza majukumu yake ya Usalama Barabarani.








Ends....







Post a Comment

0 Comments