Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la Arusha,John Kayombo ametangaza kuanza kwa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura ,kuchukua fomu pamoja za kampeni za uchaguzi, Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 Mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari mapema Leo sept 26,2024 ,ikiwa ni siku 62 za kikanuni kabla ya uchaguzi kufanyika,Kayombo ambaye pia ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha, alisema kuwa zoezi la uandikishaji katika mamlaka za wilaya ama miji litafanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu katika vituo vilivyopangwa.
Alisema zoezi la uandikishaji litawahusu wakazi wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, waliokidhi masharti ya kisheria ,wanahimizwa kushiriki uchaguzi kwa kujiandikisha ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua wagombea bora wanaowataka.
Aidha alisema wakazi wenye umri wa miaka 21 au zaidi wanaruhusiwa kugombea nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa kamati ya Mtaa kwa kuhimizwa kuchukua fomu katika ofisi za msimamizi msaidizi wa uchaguzi.
Alisema zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kugombea litafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 07 mwezi wa 11,mwaka huu katika ofisi za msimamizi msaidizi wa uchaguzi (ofisi za Mtendaji wa kata) na uteuzi wa wagombea utafanyika Novemba 8 mwaka huu.
Kayombo alisisitiza pingamizi kwa wagombea zitafanyika tarehe 8 hadi 9 mwaka huu na uamuzi wa pingamizi utatolewa kuanzia tarehe 8 hadi 10 mwaka huu kupitia ofisi ya msimamizi msaidizi.
Alisema kanuni ya 23 (3)GN .Na 574 Rufaa zote zitapokelewa kuanzia tarehe Novembe 10 hadi 13 mwaka huu na uamuzi wa kamati ya rufaa utatolewa kuanzia Novemba 10 na 13 mwak huu
Alisema kampeni za uchaguzi zinatarajia kuanza tarehe 20 hadi 26 mwaka huu kuanzia majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Kayombo alitoa rai kwa wakazi na wananchi wa jiji la Arusha kushiriki kikamilifu katika mchakato huo wa uchaguzi kuanzia hatua ya kujiandikisha hadi kupiga kura.
Alizitaja nafasi zitakazogombewa ni Mwenyekiti wa Mtaa ,wajumbe watano ambapo kati yao wawili ni wanawake,lengo ni kukuza demokrasia na kuhakikisha upatikanaji wa viongozi bora na sio bora kiongozi.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi itakayofanyika NOVEMBA 27 MWAKA HUU 2024.
Ends..
0 Comments