AMKODI OFISA IDARA YA USALAMA ,KUMUUA MKEWE NA WATOTO AWEKA DAU ZITO LA MAMILIONI,HATA HIVYO AMEJAA KWENYE MIKONO YA SHERIA

By Ngilisho Tv

Mwanaume mmoja huko Alabama Nchini Marekani amekamatwa na Polisi kwa madai ya kujaribu kukodi Mtu wa kufanya mauaji ya Mke Wake aliyeachana naye na Watoto wake sita ambao kwa sasa ni Watu wazima bila kujua kuwa Mtu huyo ni Afisa wa siri wa FBI.


Mohammad AH Mohammad, 63, ambaye taaluma yake ni Fundi na Mmiliki wa Kampuni ya American Plumbing Service, LLC amepandishwa kizimbani Ijumaa wiki hii akishtakiwa kwa jaribio la mauaji ya Familia yake mwenyewe ambayo anadai kuwa imemsaliti.


Mwanaume huyo alitafuta Mtu wa kukodisha kwaajili ya kuiangamiza Familia yake bila kujua kuwa Mtu huyo ni Afisa wa siri wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), hati za mashtaka zimeonyesha kuwa aliweka dau la $550 (Tsh. milioni 1,501,500/-) kwa kifo cha kila Mtoto wake na $20,000 (Tsh. milioni 54,437,000/-) kwa atakayemuua Mkewe.


Idara ya Polisi ya Hoover imesema kuwa Mohammad na Mkewe walianza kuwa na tofauti tangu mwaka 2022 na hadi sasa kesi yao ya talaka bado ipo Mahakamani, tangu wakati huo ametekeleza matukio kadhaa ikiwemo kumdhuru Mkewe na kuchoma moto Gari la Mtoto wake mmoja mwaka 2023.


Mohammad inasemekana kuwa alimwambia Shahidi katika kesi yake kuwa “Mungu atanilipa” ikiwa ataiangamiza Familia yake, kulingana na hati ya kiapo iliyowasilishwa Mahakamani, aliachiliwa kwa dhamana mwezi wa pili mwaka huu lakini mwezi wa nane alianza tena kutafuta Mtu wa kuiua Familia yake.


Kesi yake inaendea kusikilizwa huko Marekani na anakabiliwa na mashtaka ya kufanya jaribio la mauaji ya kukodisha.

Post a Comment

0 Comments